img

Jumla ya Tani 112 za Mchele zaangamizwa

December 1, 2020

Jumla ya tani 112 za mchele wa basmati zimeteketezwa na mamlaka ya udhibiti na usalama wa dawa na chakula baada ya kukamatwa katika ghala la Akhtar interprises maarufu simba chai liliopo Mombasa nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Tani hizo zimeteketezwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa umepitwa na muda kwa matumizi ya binadamu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa ZFDA Dkt Khamis Ali Omar wakati akitoa maelezo kuhusiana na kuteketezwa kwa mchele huo.

Amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kugundulika kuwa mmiliki wa ghala hilo anatoa mchele kwenye vifungashio vilivyomaliza muda wake tokea 2019 na kungiza   katika vifungashio vipya ambapo utatumika mpaka 2022 jambo ambalo linahatarisha afya ya mlaji.

‘’tunasikitishwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu katika  kuzibadilisha   bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi na kuziingiza katika vifungashio vipya bila ya kujali afya ya watumiaji.’’ Alisema mkurugenzi huyo.

AidhaDkt Khamis amesema ndani ya ghala hilo wamegundua tambi ambazo zishapitwa na wakati pamoja na vifuko vitupu vilivyobadilishwa mwaka kwa ajili ya kuzifunga upya ili kuanza kusambaza  katika maduka mbalimbali.

Hata hivyo Mkurugenzi amesema kwa sasa mmiliki wa Ghala hilo tayari ameshafikishwa katika vyombo vya sheri a kwa hatua zaidi.

Nae Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula ZFDA Suleiman Akida Ramadhan ameta wito kwa wananchi kuangalia na kuzichunguza kwa makini wakati wanaponunua bidhaa zao iwapo watakugundua kuna hitilafu yeyote kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika. 

Aidha amesema ZFDA itahakikisha inaendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa ambazo zipo sokoni ili kuziondosha bidhaa zilizomaliza muda kwa matumizi ya binaadamu

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *