img

Familia ya Mberesero imesema haijapokea taarifa rasmi kuhusu kifo cha kijana wao

December 1, 2020

Familia ya mtanzania anayedaiwa kujinyonga gerezani nchini, imesema mpaka sasa haijapata taarifa rasmi ya kifo cha kijana wao huyo, aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika shambulio la kigaidi la mwaka 2015 nchini Kenya.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba, Rashid Charles Mberesero, aliyekamatwa mwaka jana na wenzake wawili, alijinyonga kwa kutumia blanketi, kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *