img

Zaidi ya watu 300 washikiliwa na polisi Belarus

November 30, 2020

Zaidi ya waandamanaji 300 wamewekwa kizuizini wakisubiri kufunguliwa kesi baada ya kufanyika maandamano makubwa ya umma yasiyokuwa na kibali nchini Belarus. Hayo yameelezwa leo Jumatatu na mamlaka za nchi hiyo. 

Belarus imeshuhudia maandamano kila mwishoni mwa juma kwa takriban miezi mitano wakati upinzani nchini humo ukiendelea kupambana na juhudi zake za kutaka kumuondowa madarakani rais Alexander Lukashenko. 

Wizara ya mambo ya ndani ya Belarus imesema katika ujumbe uliotolewa kupitia tovuti kwamba jana jumla ya watu 313 walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kukiuka sheria kuhusu shughuli za mikusanyiko mikubwa. Shirika la haki za binadamu la Belarus, Viasna limsesema kiasi watu 416 wanashikiliwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *