img

Watatu wafa maji Ziwa Victoria

November 30, 2020

Watu watatu wakazi wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu ambao ni wavuvi katika ziwa victoria wamekufa maji kwa kuzama maji baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia katika shughuli zao kupasuka na kuingiza maji.

Tukio hilo limetokea jana Novemba 29 katika kata ya Kabita tarafa ya Busega wakati wavuvi hao wakiwa wanaendelea na shughuli zao za uvuvi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Richard Abwao, amewaambia waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa taarifa ya daktari aliyechunguza miili hiyo, kifo chao kilitokana na kunywa maji mengi na kukosa hewa.

“Waliokufa maji ni Mnaga Manyama miaka 28, Kulwa Juma miaka 15 na Bitulo Manyama wote wakazi wa Kabita wilayani Busega,’’ amesema.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *