img

Watano wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji

November 30, 2020

Watu watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, wakikabiliwa  na shtaka la kumuua mtu mmoja  aliyejulikana kwa jina la Jan Mathias Samuel.

Washtakiwa hao ni pamoja na Mohamed Mzee (23) mkazi wa magomeni makuti, Wilson Mauga (30) mkazi wa Kunduchi, Deus Kasuga (26) mkazi wa Mwananyamala, Yusuph Mwakalinga (30) mkazi wa Magomeni Usalama na Anderson Maloloso (49) ambae pia ni mkazi wa Magomeni Usalama.

Washtakiwa hao wamesomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Lilian Silayo na wakili wa serikali, ASP Hamis Said ambapo washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kuwa haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 14,mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa kuwa  Agosti 17, mwaka 2012 eneo la Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, washtakiwa walidaiwa kumuua mtu aliyejulikana kwa jina la Jan Mathias Samuel.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *