img

Watakaotoroka mafunzo ya mgambo mbioni kukamatwa kama waarifu

November 30, 2020

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Serikali wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe imesema ipo mbioni kutengeneza utaratibu wa kuwabana na kuwachukulia hatua kali za kisheria vijana wanaojiunga na mafunzo ya jeshi la akiba na kisha kushindwa kumaliza mafunzo hayo kwa kutoroka ili hali tayari wameshafahamu mbinu za awali za kijeshi.

Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauteri Kanoni ameyasema hayo mbele ya hadhara ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba 166 wakiwemo wanawake 21 waliomaliza mafunzo kwenye Kata ya Makoga wilayani Wanging’ombe mkoani humo ambapo amewaasa wahitimu kuwa wazalendo na nchi yao..

“Tutatengeneza utaratibu ukishajiandikisha na ukishahudhuria mafunzo,ukapata ABCD za jeshi kidogo harafu ukatoroka tutakukamata kama muarifu.Kwasababu tayari umepata siri za jeshi na sasa hivi mnatambulika kama askari na kupitia kiapo chenu mmeapa kwamba mtailinda na kuitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa”alisema  Lauteri Kanoni

Nao wahitimu wa mafunzo hayo akiwemo Josmo Mlwanda wamesema katika mafunzo hayo wamekumbana na changamoto ikiwemo ikiwemo vijana kuto tambua umuhimu wa mafunzo ya mgambo pamoja na upotoshaji kuwa mafunzo hayo ni unyanyasaji

Aidha suala la uhaba wa Sare za jeshi la akiba maarufu mgambo nalo limeonekana ni changamoto kubwa  ambapo mshauri wa mgambo wilayani Wanging’ombe, Kaptein Godwin Kimaro amesema baadhi ya wanafunzi wameshindwa kumudu ghalama za mavazi huku mkuu wa wilaya hiyo akiagiza halmashauri kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya kununua mavazi hayo.

“Naielekeza halmashauri kutenga bajeti kwa kila mwaka kwa ajili ya kununua mavazi ya askari mgambo”aliagiza Kanoni

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *