img

Wananchi wa Kata ya Naliendele walia na ukosefu wa maeneo ya kujengea huduma za kijamii

November 30, 2020

Na Faruku Ngonyani,Mtwara

Wananchi wa kata ya Naliendele iliyopo Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara wamelalamikia juu ya ukosefu wa maeneo ya kujenga maeneo ya huduma muhimu za kijamii kama vile Shule, eneo la makaburi ,Soko pamoja eneo la zahanati.

Hayo wameyazungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya kwenye Mkutano wa hadhara uliyofanyika katik eneo hilo ukiwa na lengo kwa Mkuu wa Wilaya la kusikiliza na kutatu kero za wananchi hao.

Wananchi hao wamesema kuwa kwa sasa wanakosa maeneo ya huduma ya kijamii kwa kuwa maeneo yaliyo mengi yamechukiliwa na Taasisi mbalimbali za kiserikali wakiwemo baadhi yao kiwa ni kituo cha Utafiti cha Kilimo Naliendele,Chuo cha Kilimo,jeshi la wananchi pamoja na mamlaka ya uwanja wa Ndege.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya ametoa mwezi mmoja kwa wataalam wa ardhi kutoka Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani kuhakikisha wanaenda kufanya utafiti ili maeneo hayo yaweze kupatikana na wananchi waweze kujenga nyumba za  kupata huduma muhimu za kijamii na makazi yao.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo kwa Chuo cha utafiti cha kilimo Naliendele kutoa elimu kwa wananchi wa kata hiyo ya Nalinendele ili waweze kufahamu na kujua umuhimu wa kuwa na chuo hiko katiuka eneo hilo.

Lakini pia Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito  kwa Mkurugenzi wa   Manispaa Mtwara Mkindani kutoa Notes ya miezi kwa Mtu yeyote asiyeendeleza maeneo yao na hatmae kunyang’anywa maeneo yao.

“Wale wote ambao wanamaeneo yao hayajaendelezwa  wenye hati na wasikuwa na hati kanini wasipewe notes ya kunyang’anywa maeneo hayo kwa kutoyaendeleza’’ 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *