img

Waanzilishi wa Black Lives Matter : Tulipambana kubadilisha historia na tulishinda

November 30, 2020

Dakika 5 zilizopita

Waanzilishi wa BLM

Mwaka wa 2020 utakumbukwa kwa vitu vingi – hasa kuibuka kwa harakati za Black Live Matter duniani kote.

Shirika limeongoza mikutano mikubwa ya barabarani na kampeni za hali ya juu dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi.

Sasa wanawake watatu ambao walianzisha harakati hiyo wameambia BBC wanaamini kuwa imebadilisha siasa.

“Watu weusi pamoja na washirika wetu walisimama kuibadilisha historia na tukashinda,” alisema Alicia Garza.

Garza na waanzilishi wenzake wa BLM, Patrisse Cullors na Opal Tometi, walizungumza kama sehemu ya simulizi ya wanawake 100 mwaka 2020 hafla ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao ya mahojiano makubwa na wageni tarehe 30 mwezi Novemba.

Watatu hao walianzisha harakati za Black Lives Matter mnamo mwaka 2013 baada ya George Zimmerman kukutwa hana hatia baada ya kumpiga risasi kijana mweusi ambaye hakujihami, Trayvon Martin.

Maandamano yalizuka tena mwaka huu baada ya mauaji ya George Floyd, ambaye alikufa mnamo Mei baada ya afisa wa polisi kupiga magoti shingoni mwake wakati wa kukamatwa kwake Minneapolis.

“Black Lives Matter, baada ya miaka saba, sasa iko kwenye DNA na kumbukumbu ya misuli ya nchi hii,” Garza alisema “Sote tumeangalia jinsi wanajamii wetu, wanafamilia wetu wanavyouawa kwenye kamera.

“Kuna njia nyingi ambazo, hata wakati harakati hii ilikuwa ikilipuka kwa mara ya pili, vituo vikuu vya habari vinaendelea kuzingatia jambo lisilo sahihi.

Watu wakiwa barabarani kwenye maandamano mwaka 2016 jijini New York

“Mara kwa mara, mzigo na jukumu la vurugu huwekwa miguuni mwetu, lakini hakuna mtu anayesema kuhusu vurugu ambazo jamii zetu zinapata kutoka mikononi mwa serikali, lakini pia kutoka mikononi mwa maafisa wa polisi.

Licha ya mapambano yanayoendelea, waanzilishi wa BLM wameweka matumaini, haswa wanapozungumza kuhusu kushindwa kwa Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani. Wanawake weusi haswa wamepewa sifa ya kubeba jukumu kubwa katika ushindi wa Rais mteule Joe Biden.

Opal Tometi

BBC

I think our movements are showing a whole other way is possible

Wanaharakati watatu wa vuguvugu la Black Lives Matter walipokea kutambuliwa kwao kutokana na hili na Kamala Harris, ambaye ameandika historia kama mwanamke wa kwanza mweusi na Makamu wa Rais mteule wa Marekani wa kwanza mweusi nchini humo.

Lakini walisema watamshawishi yeye asiwe tu kama “ishara lakini mpiganaji wa jamii zetu”.

“Nimefarijika kwa kuona njia ambazo harakati ya Black Lives Matter lakini pia harakati nyingine kadhaa zimeleta mawazo ya kisiasa na hatua ambazo zinaonesha vyema sisi ni nani,” Opal Tometi alisema.

“Nadhani harakati zetu zinaonesha njia nyingine inawezekana na nimeguswa sana na nashukuru kuwa hai kwa wakati kama huu.”

Familia zikishiriki katika maandamano ya watoto

Akielezea jinsi jukumu lake lilivyobadilika mwaka huu, Garza alisema Black Lives Matter inazidi kutengeneza mahusiano kote ulimwenguni, pamoja na kuyainua maandamano ya #EndSars dhidi ya ghasia za polisi nchini Nigeria.

“Tunabadilisha siasa kama tunavyoijua lakini tunazingatia sana kubadilisha nguvu, jinsi inavyofanya kazi, na kuhakikisha kuwa kuna nguvu zaidi mikononi mwa watu wengi,” alisema.

Opal Tometi, Patrisse Cullors, na Alicia Garza wakipokea tuzo ya mwaka ya Glamour Women mwaka 2016

Patrisse Cullors alisema mafanikio ya Black Lives Matter mwaka 2020 yatakuwa kwenye vitabu vya historia.

“Ninachofurahi ni kwamba mtoto wangu anasema kwamba mama yake, pamoja na wanawake wengine weusi weusi, alifanya kila kitu ambacho angeweza, na tunaweza, ili kufanya mahali hapa kuwa bora kwetu.

“Nimefurahia historia hiyo kusimuliwa.”

Wanawake 100 wa BBC hutaja wanawake 100 wenye ushawishi na wa kuvutia ulimwenguni kila mwaka, na kusimulia hadithi zao. Tufuate kwenye Instagram na Facebook na ujiunge na mazungumzo, ukitumia #BBC100Women.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *