img

Vijana kadhaa wachukuliwa mateka Libya

November 30, 2020

Vikosi vya Khalifa Hafter vimeripotiwa kubomoa baadhi ya nyumba na kuwachukuwa mateka vijana kadhaa baada ya kuvamia mji wa Ubari nchini Libya. 

Taarifa hizo za uvamizi zilizotolewa na Ofisi ya Mawasiliano ya Operesheni ya Volcano inayosimamiwa na serikali ya Libya. 

Vyanzo vya ndani pia vimefahamisha kuwa vikosi vya Khalifa Hafter vilivamia mitaa ya Al-Sharib ya mji wa Ubari ambapo viliwatishia raia kwa silaha na kuondoka wakielekea mji wa Sebha wakiwa pamoja na vijana kadhaa wa kabila la Tuareg waliowachukuwa mateka. 

Mji wa Ubari ambao ni mji wa pili kwa ukubwa baada ya Sebha katika kanda ya kusini mwa Libya, idadi kubwa ya wakazi wake inajumuisha watu wa Kabila la Tuareg. 

Kwa muda mrefu sasa nchi ya Libya ambayo imekosa utulivu, vikosi vya Khalifa Hafter vilianza kuvamia mji mkuu wa Tripoli na kudhibiti utawala baada kumarishwa na kiongozi wao Aprili 2019. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *