img

UN ina matumaini msaada wa kiutu utafika Tigray

November 30, 2020

Mkuu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi amesema ana matumaini kwamba viongozi wa serikali ya Ethiopia wataruhusu msaada wa kiutu kuingia mapema iwezekanavyo kwenye jimbo la Tigray. 

Grandi amesema bado haiwezekani msaada kupelekwa, hivyo ana matumaini jambo hilo litafanikiwa katika siku chache zijazo. Mkuu huyo wa UNHCR ameomba msaada wa kifedha kwa ajili ya kuwasaidia maelfu ya Waethiopia waliokimbilia nchi jirani ya Sudan.

 Amesema tangazo la Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kwamba amefanikiwa kumaliza operesheni za kijeshi, haimaanishi kuwa mzozo umemalizika. 

Wakati huo huo, kiongozi wa chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, Debrestsion Gebremiachel, amesema wapiganaji wake wameidungua ndege ya jeshi la Ethiopia na kuuteka tena mji wa Axum. 

Aidha, televisheni ya serikali ya Ethiopia imesema makaburi 70 yamegunduliwa katika mji wa Humera, Tigray.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *