img

Shambulizi la bomu nchini Afghanistan

November 30, 2020

Watu 31 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 24 kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa kwa kutumia gari mjini  Ghazni nchini Afghanistan.

Kulingana na taarifa za “Tolo News”, Msemaji wa Ofisi ya Gavana ya Gazne Wahidullah Jumazada alitangaza kuwa shambulizi hilo la kutumia gari la bomu lilitekelezwa karibu na jengo la usalama wa umma mjini humo.

Jumazada alibainisha kuuawa kwa watu 31, na kujeruhiwa kwa watu wengine 24 kwenye shambulizi hilo.

Katika taarifa hiyo, ilibainishwa kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa kwa kutumia gari aina ya Humvee, ambalo lilijazwa vilipuzi vilivyolipuliwa kwenye jengo hilo lililokuwa na kikosi cha makomando.

Hakuna yeyote aliyedaiwa kuhusika na shambulizi hilo hadi kufikia sasa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *