img

Serikali yasema walioajiriwa ualimu sio 13,000, yaonya waliodanganya masomo

November 30, 2020

Makatibu wakuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais Tamisemi na Ofisi ya Rais Utumishi wametoa ufafanuzi kuhusu ajira za walimu nchini.

 Hata hivyo, Katibu Mkuu Utumishi Dk Laurence Ndumbaro amesema ajira zilizotolewa ni 13,000 lakini waliopata vibali ni walimu 8000.

Dk Ndumbaro amesema pengo la walimu 5000 litazibwa wakati wowote kabla ya mwaka wa fedha 2020/21 haujaisha hivyo Watanzania hawapaswi kuwa na hofu kwa kuwa muda wa kuajiri bado upo.

“Ni kweli tulipokea maelekezo kutoka kwa Rais kuwa tuajiri walimu 13,000, lakini mfumo hauruhusu kupata ajira nyingi kwa wakati mmoja,hivyo tunakwenda kwa awamu mbili,” amesema Dk Ndumbaro.

Hata hivyo,  Katibu huyo amekiri kulikuwa na makosa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo katika mfumo hata kupelekea baadhi ya majina kujirudia mara nyingi kwenye orodha na tatizo hilo limefanyiwa kazi.

Katika hatua nyingine, Katibu ameonya walimu waliodanganya kwamba wanakwenda kufundisha masomo fulani na kupata ajira wakati wamesomea masomo mengine, watahakikiwa na watakaobainika kufanya vitendo hivyo watafukuzwa kazi mara moja na kuchukuliwa hatua zaidi ikiwemo kuzuiwa wasiingie tena katika mfumo wa ajira.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *