img

Rais wa Ujerumani awahakikishia wananchi kuhusu COVID-19

November 30, 2020

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amewahakikishia wananchi wa Ujerumani kwamba janga la virusi vya corona haliwezi kuuondoa mustakabali wao. 

Katika barua yake iliyochapishwa kwenye gazeti la Bild am Sonntag, Steinmeier amesema maendeleo kuhusu utafiti yanatoa matumaini kwamba janga la COVID-19 halitoyatawala maisha yao milele. 

Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani, Robert Koch imethibitisha maambukizi nchini humo yameongezeka hadi watu 14,611 jana Jumapili. Wizara ya afya ya Ujerumani imesema chanjo ya virusi vya corona inaweza kuidhinishwa katikati ya mwezi Desemba. 

Nchini Marekani, mkuu wa kitengo cha magonjwa yanayoambukiza Dokta Anthony Fauci, amesema maambukizi yanaweza kuongezeka wiki zijazo kutokana na sherehe za kutoa shukrani, Thanks Giving. 

Aidha, Korea Kaskazini inajenga ukuta karibu na mpaka wa Korea Kusini na inaimarisha ulinzi kwenye maeneo ya pwani ili kuzuia virusi vya corona kuingia nchini humo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *