img

Ngorongoro Heroes kibaruani leo dhidi ya Sudan Kusini

November 30, 2020

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes,  Jamhuri Kihwelo amesema kuwa anaamini vijana watafanya vizuri leo Novemba 30 kwenye mchezo dhidi ya Sudan Kusini.

Mchezo wa leo ni hatua ya nusu fainali michuano ya Cecafa ambayo inafanyika Arusha,Tanzania ikiwa ni wenyeji.

Khiwelo amesema :”Tulicheza mechi nyingi za kirafiki kwa ajili ya maandalizi na sasa tupo kwenye hatua ngumu tupo tayari kupata ushindi, imani yetu ni kwamba tutafikia lengo letu.

“Mashindano ni magumu licha ya kwamba tulifanikiwa kushinda mechi mbili mpaka kufika hapa, kikubwa ni kwamba tunajua tuna mzigo mkubwa na mzito kwa ajili ya kufikia kile ambacho tunakihitaji.

“Ushirikiano umekuwa mkubwa kutoka kwa viongozi mpaka mashabiki hili linatupa nguvu ya kufanya vizuri katika mchezo wetu,” .

Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu,Arusha.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *