img

Mzozo wa Tigray Ethiopia: Hospitali ya Mekelle yahangaika baada ya shambulio – yasema Red Cross

November 30, 2020

Dakika 7 zilizopita

Ethiopian soldiers

Hospitali kuu katika mji mkuu wa jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray inakabiliwa na “uhaba wa hatari ” wa vifaa vya matibabu huku ikiwatibu majeruhi kutoka katika maeneo ya mapigano katika mji huo, limesema shirika la msalaba mwekundu.

Jumamosi, Waziri mkuu Abiy Ahmed alisema kuwa vikosi vya muungano vimechukua udhibiti wa mji huo.

Alielezea harakati za majeshi yake kama “awamu ya mwisho ” katika mzozo wa wiki tatu na vikosi vya Tigray People’s Liberation Front.

Lakini kiongozi wa TPLF wameapa kuendelea na mapigano katika taarifa yake kwa Reuters.

Taarifa chache zimetoka Tigray katika kipindi chote cha mapigano kwasababu ya mawasiliano yamekatwa.

Taarifa kutoka katika Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu (ICRC) zinatoa mwanzo wa nadra kuhusu matukio wakati wa mzozo huo-ambapo mamia ya watu wameripotiwa kufa na maelfu wengine kuyakimbia makazi yao.

k

Shirika la msalaba mwekundu limesema nini?

ICRC ilisema magari ya ambulensi ya Shirika la msalaba mwekundu la Ethiopia yaliwabeba “majeruhi walioumia na watu waliokufa” katika hospitali ya rufaa Ayder Referral.

Walipotembelea hospitali hiyo wafanyakazi wa , ICRC walibaini “80% ya wagonjwa wenye majeraha makubwa yaliyosababisha uvujaji wa damu” na kuongeza kuwa huduma nyingine ilibidi ziahirishwe “ili wahudumu wachache waliopo na vifaa viweze kutumika kutoa huduma za dharura za matibabu “.

“Hospitali zinakabiliwa na hatari ya uhaba wa pamoja na dawa kama vile za kuua bakteria, za maumivu na glovu ,” Mkuu wa ICRC nchini Ethiopia Maria Soledad alisema.

Hospitali hiyo pia imeishiwa na mifuko ya kuhifadhia miili ya watu ,limesema shirika hilo lenye makao yake Geneva.

ICRC, hatahivyo, haikutoa takwimu zozote za idadi ya watu walioumia au kufa katika mzozo huo.

Haikutaja pia iwapo wahanga wa mzozo huo walikuwa ni raia au ni wanajeshi.

Je serikali inasema nini?

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter Jumamosi, Bw Abiy alisema kuwa jeshi limechukua udhibiti kamili wa Mekelle na hiyo “inahitiomisha awamu ya jeshi ya mwisho “.

“Ninafurahi kuwashirikisha kwamba tumekamilisha na tumesitisha harakati za kijeshi katika jimbo la Tigray,” alisema.

Aliongeza kusema kuwa jeshi liliwaachilia maelfu ya wanajeshi waliokuwa wamechukuliwa na TPLF na linadhibiti uwanja wa ndege na ofisi za jimbo, akisema kuwa mpigano yalifanywa kwa “kuwawajali raia”.

Waziri mkuu huyo amekuwa akiuelezea mara kwa mara uongozi wa TPLF kama “kikundi cha uhalifu” na alisema kuwa polisi wata “waleta katika mahakama ya sheria ”.

TPLF wamejibu nini?

Ethiopian soldiers

Katika ujumbe wake wa simu kwa shirika la habari la Reuters, kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael hakuzungumzia moja kwa moja kuhusu hali katika jimbo hilo , lakini alisema kuhusu wanajeshi wa serikali: “Ukatili wao unaweza tu kuongezea katika mapambano yetu dhidi ya wavamizi hawa mpaka mwisho .”

Aliongeza kuwa: “Hii inahusu kulinda haki yetu ya kujiamlia mambo yetu .”

Aliko Bw Debretsion hapajulikani .

Taarifa ya TPLF iliyosomwa katika televisheni ya jimbo – Tigray TV ilisema : “Mashambulio ya mabomu ya Mafashisti yamesababisha vifo vya raia na majeruhi. Serikali ya Tigray imeapa kwamba itachukua hatua za kujibu dhidi ya mashambulio ya mabomu ya kishenzi “.

Wachambuzi wanasema TPLF wanaweza kuwa wanajiandaa kurejea katika maeneo ya milimo kwa ajili ya kuanzisha mashambulio ya kuvizia dhidi ya serikali ya shirikisho.

Je kuna hofu gani ya kibinadamu?

t

Umoja wa Mataifa ulikuwa umeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa uhalifu wa kivita kama jeshi la Ethiopia lingeshambulia mji wa Mekelle.

Pia ulikuwa umeelezea wasi wasi wake kuhusu kutokuwa na uwezekano wa wahudumu wa misaada ya kiutu kuyafikia maeno yenye mzozo.

Mamlaka za Ethiopia zlisema Alhamisi kwamba “njia ya kupeleka misaada ya kiutu ” inayosimamiwa na serikali itafunguliwa, na kuongeza kuwa “wako tayari kufanya kazi na mashirika ya Umoja wa mataifa…kuwalinda raia na wale wanaoihitaji misaada hiyo”.

Pia Alhamisi, vikosi vya Ethiopia vilipelekwa katika mpaka baina Tigray na Sudan, kuwazuwia watu kuikimbia nchi, kulingana na wakimbizi.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi kuhusu hali katika jimbo la Tigray, Umoja wa Mataifa ulisema kwamba zaidi ya Waethiopia 40,000 walikuwa wamevuka mpaka tangu mzozo ulipoanza mapema mwezi wa Novemba.

Tume ya Haki za binadamu ya inayodhibitiwa na serikali ya Ethiopia ililishutumu kundi la vijana wa Tigraya kwa kuwa nyuma ya mauaji ya kikatili ya mwezi huu ambapo ilisema zaidi ya raia 600 wasio Watigray katika mji wa Mai-Kadra waliuawa. TPLF walikanusha kuhusika katika mauaji hayo.

Katika mkutano wa Ijumaa, Bw Abiy aliuambia ujumbe wa amani wa Muungano wa Afrika kuwa raia watalindwa.

TPLF ni akina nani ?

Wapiganaji wa TPLF, wanatoka katika kikosi cha kijeshi pamoja na wanamgambo waliopata mafunzo mazuri wa eneo hilo, wakikadiriwa kuwa takriban 250,000.

TPLF kilianzishwa miaka ya 1970 na kuongoza harakati zao dhidi ya utawala wa dikteta aliyekuwa na itikadi za Mimaxist Mengistu Haile Mariam, ambaye alipinduliwa mwaka 1991.

Kikundi hicho kiligeuka kuwa na msukumo wa kisiasa katika nchi hadi Bw Abiy alipochukua mamlaka na kuwa Waziri Mkuu mwaka 2018.

Bw Debretsion alisema kuwa vikosi vya Tigray viko “tayari kufa vikilinda haki yetu ya kutawa jimbo letu “.

Mapigano ni ya nini ?

An Ethiopian soldier

Mzozo wenye mizizi ya muda mrefu ya uhasama baina ya serikali ya Ethiopia na TPLF, uliibuliwa tena na hatua za Bw Abiy za kukitenga chama.

Wakati Bw Abiy alipoahirisha utaguzi wa kitaifa kwasababu ya virusi vya corona mwezi Juni, mahusiano yalizorota zaidi.

TPLF ilisema kuwa muda wa serikali wa kuongoza umeisha, ikidai kwamba Bw Abiy hajajaribiwa katika uchaguzi wa taifa.

Mwezi wa Septemba chama kilifanya uchaguzi wake , ambao serikali ilisema kuwa “haukuwa wa kisheria “.

Mapema mwezi wa Novemba, wapiganaji wa TPLF waliingia katika ngome ya jeshi katika mji wa Mekelle ambao ulikuwa ndio mwanzo wa harakati za majeshi ya muungano katika jimbo

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *