img

Mwalimu muuaji wa Al-Shabab auawa kwa risasi

November 30, 2020

Mwalimu na wanaume wengine wawili wameuawa kwa kikosi cha ufyatuaji risasi Somali baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kutekeleza mauaji kwa niaba ya kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Vifo vyao ni agizo la mahakama ya jeshi katika mji wa Mogadishu.

Mohamed Haji Ahmed alikuwa mwalimu wa lugha ya Kiingereza katika chuo kikuu cha Mogadishu.

Pia alikuwa muuaji aliyetumwa na al-Shabab – na alitekeleza mauaji ya maafisa wa ngazi ya juu serikalini.

Pia alielezewa kama “muuaji asiye na huruma” – na kushutumiwa kwa kuwa mkuu wa kikosi cha eneo cha mauaji kilichoendeshwa na kundi la al-Shabab mjini Mogadishu na eneo la Benaadir.

Pamoja na wanaume wengine wawili, aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili asubuhi.

Mwanaume huyo, 27, alipatikana na hatia ya mauaji ya Jenerali Gen Abdullahi Mohamed Sheikh mwaka 2017, naibu mkuu wa sheria Mohamed Abdirahman Mohamud mwaka 2019 na jenerali polisi Mohamud Haji Alow baadaye mwaka huo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *