img

Museveni ashutumu wanasiasa wa upinzani kupotosha vijana

November 30, 2020

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshutumu waandamanaji na wanasiasa wa upinzani kwa kuwapotosha vijana kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

Bwana Museveni amesema wazo la kuwa mheshimiwa Bobi Wine akikamatwa kutakuwa na ghasia lisirejee tena.

‘’Hakuna mwanasiasa ambaye ana mamlaka kuliko sheria’’, Museveni alisema.

Aliongeza kuwa wanasiasa wanalipa magenge ya uhalifu ambao wametangaza baadhi ya sehemu za mji wa Kampala eti hazitawaliki na hata kuvamia maafisa wa polisi wanaoshika doria.

Bwana Museveniameshutumu watu waliorekodiwa wakivamia maafisa wa usalama na waliokuwa wamevaa mavazi ya rangi ya njano inayoashiria chama tawala.

‘’Hili, halitawahi kutokea tena, kwasababu waliotekeleza hayo wameona matokeo ya kucheza na moto’’, amesema rais Museveni.

Bwana Museveni pia alisema kuwa ajenda za wanasiasa wa upinzani ni kupata uungwaji mkono kutoka nje ya nchi ambao nia yao ni kukosesha uthabiti nchi ya Uganda.

Rais Museveni aliongeza kuwa makosa makubwa ni wagombea urais walikiuka hatua zilizowekwa za kukabiliana na virusi vya corona na kutojali utekelezaji wa sheria.

Pia, alitoa risala zake za rambirambi kwa raia wa Uganda waliopoteza wapendwa wao wakati wa ghasia hizo na kuongeza kwamba serikali itawalipa fidia.

Bobi Wine anatafuta kumuondoa madarakani Museveni ambaye ametawala nchi hiyo kwa miaka 34 – katika uchaguzi utakaofanyika Januari 2021.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *