img

Mpambano wa Mike Tyson dhidi ya Roy Jones Jr umeshindwa kumpata mbabe

November 30, 2020

 Mpambano wa masumbwi ambao ulikuwa wa hisani, baina ya Bingwa wa zamani wa Ndodi, Mike ‘Iron’ Tyson dhidi ya Roy Jones Jr umeshindwa  kumpata mbabe baada ya majaji kutangaza kuwa ni droo, mpambano huo ambao ulikuwa wa raundi nane, ulipigwa mwishoni mwa wikiendi jijini Los Angeles Marekani.

Mike Tyson, (54) ambaye ubingwa wake wa kwanza aliupata Miaka 36 iliopita baada ya kumtwanga Trevor Berbick, Las Vegas mwaka 1986 na kuweka rekodi ya kuwa bingwa wa uzani wa juu (Heavy weight) mdogo kutwaa mkanda huo.

Muda mwingi wa pambano hilo #RoyJones alionekana kuzidiwa na makonde aliyokuwa anarushiwa na Tyson.

Majaji waliwashangaza wengi, baada ya kutangaza matokeo kuwa ni sare, kwani wengi walidhani Tyson ameshinda kwa jinsi alivyotawala pambano hilo ambalo halikuwa la Ubingwa.

Tyson mara baada ya pambano alisema alikuwa anaona dakika mbili ni nyingi hiyo ni kutokana kutopanda ulingoni kwa muda kwa muda mrefu  pambano lake mwisho lilikuwa mwaka 2005 ambalo alipoteza dhidi ya Kevin McBride kwa KO na kuamua kutangaza kustaafu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *