img

Mohsen Fakhrizadeh: Je nini chanzo cha mauaji ya mwanasayansi huyu wa Iran?

November 30, 2020

Dakika 8 zilizopita

Mohsen Fakhrizadeh

Alikuwa hana umaarufu nchini Iran hadi Ijumaa iliopita wakati alipouawa. Mwanasayansi huyu Mohsen Fakhrizadeh alikuwa mtu maarufu tu kwa wale waliofuatlia mpango wa kinyuklia wa Iran .

Vyanzo vya usalama vya magharibi vilimchukulia kama mtu muhimu sana.

Vyombo vya habari vya Iran vilipuuzilia mbali umhimu wa bwana Fakhrizadeh, vikimtaja kuwa mwanasayansi na mtafiti anayehusika na kifaa cha kupima Covid 19 katika wiki za hivi karibuni.

Mark Fitzpatrick , mshiriki katika taasisi ya kimataifa kuhusu mafunzo ya kimkakati mjini London ambaye anafuatilia sana mpango wa kinyuklia wa Iran , alituma ujumbe wa twitter akisema: Mpango wa kinyuklia wa Iran utakuwa umepita mpaka wake iwapo utakuwa ukimtegemea mtu mmoja.

Wakati tunajua kwamba wakati aliposhambuliwa Fakhrizadeh aliandamana na walinzi kadhaa , ikiashiria jinsi Iran ilivyochukulia umuhimu wa usalama wake.

Hivyobasi lengo la mauaji yake – ambayo hakuna hata mtu mmoja aliyekiri kutekeleza – huenda yamefanyika kisiasa badala ya uhusiano wake wa mipango ya kinyuklia ya Iran.

Malengo mawili ya mauaji yake yanaonekana. Kwanza kukandamiza kuimarika kwa Uhusiano kati ya Iran na utawala mpya wa rais mteule Joe Biden nchini Marekani. Na pili, kuishinikiza Iran kuanza harakati za kutaka kulipiza kisasi.

”Maadui wanakabiliwa na majuma yenye shinikizo kali” , alisema rais wa Iran Hassan Rouhani katika matamshi yake ya kwanza kuhusu mauaji hayo.

”Wana wasiwasi kwamba hali duniani inabadilika na wanajaribu kutumia muda uliosalia kuleta hali tete katika eneo letu”, aliongezea.

Wakati bwana Rouhani anapowataja maadui wa Iran anazungumzia kwa Ushahidi kuhusu utawala wa rais Trump , Israel na Saudia.

Israel na Saudia zina wasiwasi kuhusu mabadiliko ya kisiasa katika Eneo la mashariki ya kati na athari zake kwao wakati rais mteule Joe Biden atakapochukua madaraka.

Bwana Biden alisema wazi kwamba angependelea kujiunga tena katika mazungumzo ya mpango wa Kinyuklia wa Iran , ambao ulifanywa na aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama 2015 na kufutiliwa mbali na Donald Trump 2018.

Eeneo ambalo mauaji yalifanyika

Maelezo ya picha,

Fakhrizadeh alijeruhiwa katika shambulio hilo na kufariki hospitalini

Wasiwasi wa Israel na Saudia kuhusu Iran ulijadiliwa katika kile ambacho vyombo vya habari vya israel vinasema ulikuwa mkutano wa siri kati ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman katika eneo la Neom siku ya Jumapili.

Waziri wa masuala ya kigeni nchini Saudia alikana kwamba mkutano huo ulifanyika. Bwana Netanyahu alidaiwa kwamba hakufanikiwa kumshawishi mwanamfalme huyo kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Siku ya Jumatatu , wakati Iran ilipounga mkono waasi wa Houthi nchini Yemen waliposhambulia hifadhi moja ya mafuta inayomilikiwa na kampuni ya mafuta ya Aramco karibu na bahari ya shamu huko Jeddah, uwezekano wa kuzungumza na Saudia ulikuwa umejitokeza.

Vyombo vya Iran vyenye misimamo mikali vilisifu kombora la Quds 2 lililorushwa na wasi wa Houthi.

Ulikuwa mpango wa kimkakati , uliopangwa ili kuingiana na mkutano wa Saudia na Israel, ukiwaonya wasipuuze hatua yao, kilisema chombo cha habari cha Mehr.

Hasira za Saudia kuhusu shambulio hilo pia zilisikika Marekani.

Mshauri wa kitaifa kuhusu masuala ya Usalama nchini humo John Bolton alielezea katika kitabu chake , Chumba ambacho yote yalifanyika , jinsi utawala wa Trump ulivyotazama Iran ikiunga mkono Waasi wa Houthi ikiwa ni kampeni dhidi ya Marekani katika eneo la mashariki ya kati.

Mkutano huo wa Neom ulidaiwa kupangwa na waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo , ambaye alikuwa amekwenda Qatar na UAE , ambapo Iran ndio iliokuwa ajenda kuu.

Wiki mbili mapema , rais Trump alikuwa amewaomba washauri wake wakuu iwapo alikuwa na mbadala wa kushambulia maeneo ya kinyuklia ya Iran , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani .

Alionekana kutaka kuikomesha Iran kabla hajaondoka madarakani.

Mnamo mwezi Januari , bwana Trump alijisifu kuhusu mauaji ya kutumia ndege isio na rubani nchini Iraq dhidi ya kiongozi mkuu wa jeshi la Iran jenerali Qasem Soleiman, licha ya kutangazwa na mwakilishi maalum wa umoja wa mataifa kuwa kinyume na sheria

”Tulimzuia haraka na tulimuua kwa kufuata agizo langu”, alisema.

Hivyobasi huenda ikadaiwa kwamba mauaji hayapingwi na rais. Mwenzake wa Iran aliilaumu Israel kwa kufanya mauaji ya Fakhrizadeh.

Na kweli ripoti nyingi zinasema kwamba waziri mkuu Netanyahu alikuwa miongoni mwa viongozi wachache duniani waliozungumza kuhusu mwanasayansi huyo.

Katika hotuba ya moja kwa moja katika runinga 2018 , alizungumza kuhusu jukumu la Fakhrizadeh katika mpango wa kinyuklia wa Iran na kuwaambia watu ‘kulikumbuka jina hilo’.

Huku Israel ikiwa na Imani na kujua kwamba Marekani italilinda taifa hilo chini ya uongozi wa Biden , ina wasiwasi kwamba chaguo lake la waziri wa masuala ya kigeni Antony Blinken anaunga mkono mpango wa kinyuklia wa Iran.

Jinsi Bwana Blinken anavyotazama hali ilivyo mashariki ya kati , pia kunaweza kusababisha fursa nyingi kwa Wapalestina.

Alikuwa mkosoaji mkuu wa Trump kuhamisha ubalozi wa Marekani kuelekea Jerusalem kutoka Tel Aviv, licha ya kwamba bwana Biden amesema kwamba hatouridisha ubalozi huo ulikotoka.

Kiongozi wa kidini nchini Iran , Ayatollah Ali Khamenei, ametaka wale waliohusika na mauaji ya mwanasayansi huyo kuadhibiw

Kiongozi wa baraza la ufanisi la Iran Mohsen Rezaei amedai kwamba kuna ukosefu wa usalama.

“Kitengo cha ujasusi cha Iran kinapaswa kugundua wavamizi na vyanzo vya upelelezi vya kigeni na kusitisha mauaji”, alisema.

Raia wengi wa Iran katika mitandao ya kijamii wameuliza ni vipi licha ya kujisifu kuwa na uwezo wa kijeshi na ujasusi , mtu anayelindwa sana anaweza kuuawa mchana.

Pia kuna wasiwasi kwamba mauaji hayo yatatumika kama sababu ya kuwakamata watu nchini humo.

Sasa kwamba utawala wa rais Trump unaondoka madarakani na Israel na Saudia wanakosa mshirika wao mkuu, Iran inatazamia uwezekano wa kuondolewa vikwazo na utawala wa Biden na fursa ya kujenga upya uchumi wake.

Hivyobasi itaharibu iwapo itaamua kulipiza kisasi.a.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *