img

Mfahamu Kim Kardashian kiundani zaidi

November 30, 2020

Oktoba 21, 1980 alizaliwa mwigizaji, model, mfanyabiashara na mhusika katika vyombo vya habari Kim Kardashian.

Jina lake halisi ni Kimberly Noel Kardashian West. Alizaliwa huko Beverley Hills, Los Angeles katika jimbo la California nchini Marekani kwa wazazi Robert Kardashian na Kris Jenner.

Ana ndugu zake wengine Kourtney, Khloe na Rob. Mama yao ana asili ya Udachi, Uingereza, Uskochi na Ireland. Baba yake ni kizazi cha tatu chenye asili kutoka Armenia waliozamia nchini Marekani. Baada ya wazazi wake kuwa wadaawa tangu mwaka 1991, mama yake aliolewa na Bruce Jenner ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 1976 katika decathlon.

Kutoka hapo Kim alipata ndugu wengine Burton mwiite Burt, Brandon na Brody pia Casey, Kendall na Kylie Jenner ambao wote hawa ni wasanii wa muziki nchini humo. Baba yake kabla hajafariki dunia, enzi za uhai wake alijikita katika masuala ya sheria na biashara. Hii ndio sababu baba yake anachukuliwa kuwa mwanzilishi wa kampuni la Movies Tunes Inc. ambayo ilijikita katika muziki na masoko.

Hivyo haishangazi kumuona Kim akijikita katika masoko. Kim alisoma katika shule ya Kikatoliki ya wasichana ya Marymount huko Los Angeles. Mnamo mwaka 1994 baba yake alikuwa wakili wa mchezaji wa mpira O.J Simpson katika tuhuma za mauaji zilizokuwa zikimkabili.

Baba yake alifariki dunia mwaka 2003 kwa maradhi ya saratani. Kim akiwa na miaka 20 alikuwa karibu sana na mwanamitindo Paris Hilton hali iliyomfanya ajulikane zaidi katika vyombo vya habari. Kim ameonekana katika filamu nyingi zikiwamo Disaster Movie (2008), Deep in the Valley (2009) na Temptation: Confessions of a Marriage Counselor (2013). Jarida la Time lilimtaja katika orodha ya watu 100 wenye ushawishi duniani.

Kim ni mke wa msanii wa Hip Hop Kanye West miezi sita iliyopita Kanye na Kim Kardashian walikuwa wakizungumzia kuzaa mtoto wanne.
,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *