img

Mamia ya wafuasi wa upinzani wakamatwa Pakistan

November 30, 2020

Polisi nchini Pakistan wamewakamata mamia ya wafuasi wa vyama vya upinzani kabla ya kufanyika mkutano mkubwa wa hadhara uliopangwa leo jumatatu wa kumshinikiza waziri mkuuu ajiuzulu. Serikali imetetea hatua ya kukamatwa wafuasi hao wa upinzani ikisema inahitajika katika kupambana na janga la virusi vya Corona. 

Polisi imekiri kuwakamata zaidi ya watu 370 wakati ambapo vyama vya upinzani vinasema waliokamatwa ni zaidi ya watu 1800 katika mji wa Multan nchini Pakistan.

Upinzani umesema mamkala katika eneo hilo imefunga mtandao wa simu katika eneo zima. Vikosi vya usalama vilipanga makontena makubwa katika barabara kuu za eneo hilo jana Jumapili usiku kuzuia njia ya kuelekea kwenye uwanja wa bustani ya umma ambako wapinzani walipanga kuandamana dhidi ya waziri mkuu Imran Khan. 

Miongoni mwa waliokamatwa ni Ali Musa Gillani mwanawe waziri mkuu wa zamani Yousaf Raza Gilani.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *