img

KMC FC yajipanga katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Disemba Nne

November 30, 2020

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC inaendelea kujifua kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Timu ya Dodoma Jiji utakaopigwa Disemba Nne mwaka huu katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, KMC FC ambao ni wenyeji, wanafanya maandalizi  katika uwanja wa White Sand Hotel ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mipango na mikakati ya kupata ushindi huo unafanikiwa kwa asilimia kubwa ilikuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara  msimu wa 2020/2021.

Kikosi cha KMC FC ambacho kinanolewa na makocha wawili wa zawa ambao ni John Simkoko pamoja na Habibu Kondo, kimejipanga kuhakikisha kwamba kinaendeleza ushindi ikiwa ni baada ya kumfunga Azamu goli moja kwa bila na hivyo kupata alama tatu katika uwanja wa Uhuru Novemba 22 mwaka huu.

“ Kikosi chetu kipo imara, hatuna majeruhi, tunaimani kwamba maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika yataleta matokeo mazuri katika mchezo huo,na mingine ambayo tutacheza pia, hatujiandai kwa ajili ya mechi moja,ila ni kwa kila mechi ambazo zipo mbele yetu”.

 Hatujacheza michezo miwili dhidi ya Namungo pamoja na Simba, kwa hiyo tumekuwa na wakati mzuri zaii  wakufanya maandalizi yetu, hivyo mashabiki wategemeekuona Pira Spana tukiliendeleza kwa wapinzani wetu.

Hata hivyo KMC FC mbali na kucheza na Dodoma Jiji, pia itakutana na Mtibwa Suger mchezo ambao utapigwa mkoani Morogoro,  Ihefu Mbeya pamoja na JKT Tanzania katika uwanja Samora Iringa.

Mbali na michezo hiyo, KMC FC bado itakuwa na viporo vya michezo miwili ambayo ni dhidi ya Namungo pamoja na Simba timu hizo kwa sasa zinashiriki michuano ya kimataifa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *