img

Kenya na Somalia zashikana mashati kuhusu jimbo la Jubbaland

November 30, 2020

Dakika 2 zilizopita

Rais wa Somali kushoto na mwenzake wa Kenya walipokutana jijini Nairobi

Kenya imesema kwamba haijapokea ilani yoyote inayoitaka kumrudisha nyumbani balozi wake nchini Somalia kufuatia madai ya kuingilia masuala ya ndani na yale ya kisiasa ya taifa hilo.

Nairobi pia ilipinga shutuma hizo ikizitaja kuwa zisizo na Ushahidi wowote.

Katika taarifa , wizara ya masuala ya kigeni nchini Kenya imesema kwamba inaunga mkono kuimarika kwa Somalia na kuonya kwamba hatua hiyo huenda ikaathiri mchakato wa Mogadishu katika kujijenga upya.

”Serikali ya Kenya inaheshimu na kufuata sheria za kimataifa za uhuruwa kitaifa ,ule wa kieneo na pia kisiasa hususana kwa mataifa Afrika”.

Hatua hiyo ya Kenya inajiri baada ya Somalia siku ya Jumapili kumtaka balozi wake nchini Kenya Mohamud Ahmed Nur ‘Tarzan’ kurudi nyumbani kwa mazungumzo baada ya kuishutumu Kenya kwa kuingilia masuala yake ya nyumbani.

Mogadishu pia iliagiza balozi wa Kenya nchini Somalia Lucas Tumbo kurudi Nairobi.

Inadaiwa kwamba tangazo hilo lilitolewa baada ya bwana Nur Kuwasili nyumbani Mogadishu.

Suala la Jubbaland

Bwana Nur , katibu wa kudumu katika wizara ya masuala ya kigeni nchini Somalia , alinukuliwa na chombo cha habari cha taifa hilo akisema kwamba Kenya ilimshawishi kiongozi wa jimbo la Jubbaland Ahmed Islan Madobe , kukaidi makubaliano muhimu ya kisiasa.

Makubaliano kati ya majimbo hayo na serikali hiyo ya kijimbo yalioafikiwa miezi miwili iliopita yanahusu mpango wa kufanya uchaguzi usio moja kwa moja wa wabunge katika miji mikuu ya kila jimbo.

Serikali ya Somalia inaelewa kwamba kutokana na hatua ya serikali ya Kenya katika kuingilia masuala ya kisiasa ya taifa la Somalia , Rais wa Jimbo la Jubbaland ameenda kinyume na makubaliano yalioafikiwa tarehe 17 Septemba mjini Mogadishu, katibu huyo alisema siku ya Jumapili.

Moja ya makubaliano hayo ya kisiasa yalimaanisha kwamba vituo viwili vya mji katika kila jimbo vitatumika kama vituo vya kupigia kura kuwachagua wabunge.

Lakini Jubbaland ilitofautiana na serikali hiyo ya kijimbo kuhusu iwapo jimbo hilo litasimamia kamili usalama wa vituo hivyo.

Pia walitofautiana kuhusu vituo hivyo. Siku ya Jumapili, Madobe alionya kwamba hakutakuwa na uchaguzi katika jimbo lake hadi suala hilo litakapotatuliwa haraka iwezekanavyo.

Lakini Kenya inasema kwamba ilikuwa ikizishinikiza pande zote kufanya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika.

”Ni jukumu la pande zote za kiaisa nchini Somalia kuafikia majukumu yake ya kisiasa kuzuia hatua zinazoweza kuficha yanayoendelea na kufanya mazungumzo ya kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa muda uliowekwa , hatua ambayo itaadhimisha wakati muhimu wa juhudi za ujenzi wa Somalia”.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *