img

Katambi awataka Shinyanga kukaa mkao wa kula

November 30, 2020

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi amesema atahakikisha anashirikiana na madiwani wote wa manispaa ya Shinyanga ili kuhakikisha ahadi zote alizoziahidi na zilizoahidiwa na madiwani zinatekelezwa kwa wakati.

Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini humo, ambapo aliwataka wananchi wakae mkao wa kula kwa utekelezaji wa ahadi hizo.

Amesema hatakuwa tayari kucheka na mtu ambaye hatakuwa tayari katika kutekeleza yale yaliyoahidiwa katika sekta yote, kwani  kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kero zilizopo kwenye kata zao  zinasimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

“Sasa kazi tunaianza yale yote tuliyokuwa tumeyaahidi tutayafanya na tuko tayari kuwatumikia wananchi wakati wote usiku na mchana ili kuhakikisha manispaa inabadilika, inakuwa na maendeleo zaidi hatutakubali kurudi nyuma tunataka tusonge mbele”amesema Katambi.

Katambi amesema atahakikisha anasimamia sekta ya kilimo akianzia zao la pamba na wataongeza mazao mengine ya biashara ili kuweza kuongeza uchumi wa manispaa ya Shinyanga.

Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga Daved Nkulila amesema baraza la madiwani analoenda kuliongoza ataliongoza vyema na kuhakikisha madiwani wote wanasimamia kazi zao kikamilifu.Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Abubakar Mkadam amesema wanaendelea kupanga mkakati ili kuona ni namna gani  madiwani wataondoa kero zilizopo kwa kushirikiana na mbunge bega kwa bega.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *