img

Yafahamu magonjwa ambayo ukiyapata yanakuwa ya kudumu

November 29, 2020

Dakika 4 zilizopita

Agogo da magunguna

Kuna baadhi ya magonjwa ambayo binadamu akiyapata hayawezi kamwe kupona, kulingana na wataalamu wa afya. Mengi kati ya magonjwa haya hayana uhusiano na tofauti za umri, na baadhi yana uhusiano wa moja kwa moja na umri wa mtu.

Wakati mwingine baadi ya magonjwa hurithishwa watoto lakini kuna mengine ambayo hayarithishwi kutoka kwa wazazi na unapoyapata huwezi kupona.

Tuangalie baadhi ya magonjwa hatari zaidi kwa maisha ya binadamu:

Ugonjwa wa figo

Figo zimeumbwa kuwa mbili. Kazi yake ni kuchuja maji machafu yanayotoka katika sehemu nyingine za mwili na kusafisha damu chafu na uchafu huo huenda moja kwa moja kupitia njia ya mkojo.

getty

Hali hii ina maana kwamba figo zitakuwa hazifanyi kazi ipasavyo.

Ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu ndio magonjwa hatari zaidi.

Tatizo hili linaweza kutibiwa kwa njia ya upandikizaji wa figo au kwa kusafisha figo mara kwa mara.

Unaweza kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa figo kama una magonjwa yafuatayo:

 • Shinikizo la damu
 • Kisukari
 • Kiharusi
 • Kama ulishawahi kupata maambukizi ya figo

Baadhi ya mambo yanayoweza kusaidia kujiepusha na maradhi ya figo:

 • Punguza kiwango cha chumvi unayokula
 • Kula mboga za kijani kibichi
 • Fanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara
 • Acha unywaji wa pombe na kuvuta sigara

Pumu (Asthma)

Shirika la afya duniani linasema maradhi ya pumu huwaathiri watu wa kila rika

Ni ugonjwa unaomfanya mtu asipumue vyema.

Lakini maumivu anayoyapata mgonjwa huendelea na huja ghafla wakati mwingine hudumu kwa saa kadhaa na hata muda mrefu zaidi.

Getty

Maelezo ya picha,

Kushindwa kutumia kifaa kunaweza kusababisha kifo

Hali hii huathiri mfumo wa kupumua unaohusiana na mapafu na hii inaweza kusababisha mgongwa kuwa na hali mbali.

Utafiti wa hivi karibuni ulibaini kuwa wengi miongoni kwa wagonjwa wa pumu hawatumii kifaa cha kudhibiti ugonjwa huu kwa ufanisi wakati mgonjwa anapokuwa katika hali ya dharura.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha utafiti wa maradhi ya pumu -UK Asthma Research Center, ulibaini kuwa wagonjwa wa pumu wengi walikuwa hawajafundishwa jinsi ya kutumia kifaa cha kupumulia wanapokuwa katika hali ya dharura.

Kwa mujibu wa utafiti huo, wagonjwa walikuwa wanachanganyikiwa wanapoanza kukitumia.

Unaweza pia kusoma:

Shikizo la damu

Shikizo la damu ni ugonjwa unaosababisha kuziba kwa mishipa fulani ya damu inayopeleka ujumbe kwenye ubongo na mara inaposhindwa kufanya kazi inaleta matatizo.

Shirika la afya duniani (WHO) linasema katika ripoti yake kwamba kuna watu milioni 1.13 wanaoishi na maradhi ya shinikizo la damu kote duniani na theruthi mbili ni watu wanaoishi maisha ya kiwango cha kati.

Mwaka 2015 utafiti wa WHO ulibaini kuwa mwanaume 1 kati ya wanaume 4 anaishi na ugonjwa huu, huku mwanamke 1 kati ya wanawake 5 akiwa na maradhi haya.

Shinikizo la damu ni ugonjwa mbaya ambao hauwezi kutibiwa unapogundulika kuwa nao.

Getty

Maelezo ya picha,

Kuna vitu vinavyochochea mtu kupatwa na ugonjwa huu

Mambo yanayosababisha shinikizo la damu:

 • Kuongezeka kwa ukubwa na uzito wa mwili
 • Msongo wa mawazo
 • Unywaji wa pombe
 • Ulaji wa chumvu nyingi
 • Maradhi ya ubongo ya Alzheimer
 • Ulaji wa vyakula vya mafuta
 • Kutopumzika vya kutosha hasa usiku
 • Ukosefu wa mazoezi ya mwili
Getty

Ugonjwa wa kisukari

Kulingana na utafiti na wataalamu mbali mbali matumizi ya sukari huchangia katika kuchochea mtu kupata maradhi ya kisukari.

Kuna aina za Kisukari (Diabetes).

Kuna aina ya kwanza ya kisukari inayofahamika kama – Type 1- ambao mara nyingi watu wanaoupata huwa hawajaurithi kutoka kwa watu wa vizazi vya awali vya familia zao.

Aina hii ya kisukari mara nyingi huwapata watoto au vijana walio katika miaka 20 na chini ya miaka hiyo.

Wenye ugonjwa huu ni wachache duniani “kwasababu idadi yao haizidi watu milioni 1.2 kote duniani ,” anasema dokta Salihu Kwaifa kutoka Nigeria.

Wenye aina hii ya kisukari huwa hawana sukari ya mwili (insulin) ya kutosha, na dalili zake zinatambuliwa haraka kama vile kupata haja ndogo mara kwa mara kiu na unywaji wa maji wa mara kwa mara kulingana na wataalamu.

Kuna aina ya pili ya kisukari inayofahamika kama -Type 2 -aina hii huwapata watu wengi hususan watu wenye umri wa miaka kati ya 20 na 79.

Wataalamu wanakadiria kuwa kuna watu wapatao milioni 560 wanaoishi na aina hii ya kisukari duniani.

Maumivu ya mifupa

getty

Ugonwa huu husababishwa na maambukizi yanayoshambulia supu ya mfupa na huwapata watu kwa njia mbali mbali.

Wakati mwingine maambukiz haya husababishwa na bakteria ambao hutengeneza kimiminika katika eneo lililoathiriwa na wakati mwingine hutokea mtu anapopata jeraha alipokuwa mtoto na jeraha hilo kuongezeka anapokuwa katika umri wa utu uzima na jeraha hilo kurejea tena.

Ugonjwa huu unajitokeza kwa aina nyingi kuna matibabu ya awali ambayo huitwa Acute Arthritis ambayo hudumu kwa miezi miwili na ni rahisi kupona.

Kwa arthritis ya kudumu, kwa kawaida matibabu huchukua miezi sita au zaidi zaidi kwa mtu kupata nafuu.

Hakuna dawa inayotolewa hospitalini inayoweza kutibu maradhi haya, japo athari zake zinaweza kutulizwa.

Mambo yanayochangia zaidi maumivu

Umri: Ugonjwa huu unaweza kumuathiri mtu yoyote lakini mara nyingi kuwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 60.

Jinsia : Theruthi mbili ya maambukizi mapya ya ugonjwa huu huwapata wanawake, kwahiyo wana hatari zaidi ya kuupata kuliko wanaume.

Urithi : Watu waliozaliwa na aina mbali mbali za matatizo ya kiafya wana hatari ya kupatwa na ugonjwa huu wa mifupa.

Uvutaji wa sigara: Tafiti zinaonesha kuwa uvutaji wa sigara unaweza kusababisha ugonjwa huu, na kuufanya uwe mbaya zaidi.

Uzazi : Wanawake ambao hawazai wanakabiliwa na hatari kubwa kuliko waliozaa.

Unene na uzito wa mwili wa kupita kiasi: Ukubwa wa mwili unahusishwa na matatizo mbali mbali ya afya. Kuna kitu kimoja kinachopunguza hatari ya maambukizi kwa mwanamke- Kunyonyesha kunapunguza hatari ya maambukizi kwa mwanamke, wanasema wataalamu wa afya.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *