img

Wafanyakazi wa mashamba ya mpunga wauawa kwa “kuchinjwa” Nigeria

November 29, 2020

Dakika 2 zilizopita

The 43 farmers were buried on Sunday

Maelezo ya picha,

Wakulima 43 wamezikwa Jumapili

Watu karibu 43 wameuawa katika kile ambacho rais wa Nigeria anakieleza kama shambulizi la “kiwenda wazimu” lililotekelezwa kaskazini mashariki mwa Nigeria Jumamosi.

Washambuliaji waliwafunga kamba wafanyakazi wa mashamba ya mpunga na kukata koo zao karibu na eneo la Maiduguri, mji mkuu wa Borno, ripoti zinasema.

Hili lilikuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni ambako makundi ya wanamgambo wa Boko Haram na Islamic State Magharibi mwa Afrika yanatekeleza shughuli zake.

Hadi kufikia sasa hakuna aliyedia kuhusika na shambulizi hilo.

“Nalaani mauaji ya wakulima wetu ambao ni wachapa kazi yaliyotekelezwa na wanamgambo katika jimbo la Borno. Nchi nzima imeumizwa na mauaji haya. Maombi yangu ni kwa familia katika kipindi hiki kigumu cha maombelezi. Mungu alaze roho zao mahali pema peponi,” amesema Rais Muhammadu Buhari.

Rais Buhari pia alielezea “mauaji hayo ya kigaidi kama uendawazimu”, kulingana na msemaji wake Garba Shehu.

White spacer

“Tumepata miili 43 ya watu waliokufa, wote wamechinjwa pamoja na wengine sita waliopata majeraha mabaya,” afisa wa polisi wa eneo aliyesaidia walionusurika amezungumza na shirika la habari la AFP.

Baadhi ya wafanyakazi wa mashamba hayo bado hawajulikani walipo, huku mkaazi mmoja na Shirika la Amnesty International wakisema wanawake 10 ni miongoni mwao.

Waathirika wa shambulizi hilo ni wafanyakazi wa mashamba kutoka jimbo la Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria.

The governor of Borno state (CR in the background, with yellow hat and white and yellow robe) attended the victims' funerals on Sunday

Maelezo ya picha,

Waliofariki dunia wamezikwa Jumapili, gavana wa jimbo akihudhuria mazishi hayo

Gavana wa jimbo la Borno, Babagana Zulum, alihudhuria’ mazishi ya waaathirika Jumapili.

“Inaumiza moyo kuona zaidi ya raia 40 wamechinjwa wakiwa wanafanyakazi katika mashamba yao,” aliwaambia wanahabari.

“Watu wetu wanapitia kipindi kigumu sana, njia mbili tofauti: upande mmoja wakisalia nyumbani, huenda wakafariki dunia kwasababu ya njaa; na upande mwingine, wanakwenda kufanyakazi yao ya shambani na wanakuwa katika hatari ya kuuliwa na wanamgambo. Hii inasikitisha sana.”

Alitoa wito kwa serikali kusajili wanajeshi zaidi na maafisa wengine wa usalama kulinda wakulima katika eneo hilo.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *