img

Uturuki yalaani mauaji ya Mwanasayansi wa Iran Mohsen Fakhrizadeh

November 29, 2020

Wizara ya mambo ya kigeni ya Uturuki imelaani mauaji ya mwanasayansi aliyehusika na programu ya silaha za kijeshi nchini Iran Mohsen Fakhrizadeh kwa kuyaita “mauaji ya chuki.

” Uturuki inatumai waliohusika na mauaji hayo watakabiliwa na mkono wa sheria, huku ikitoa wito wa utulivu na kutaka vyama vya kikanda kuacha kuchukua hatua au misimamo itakayosababisha mivutano.

 Fakhrizadeh alipigwa risasi katika shambulizi lililotokea siku ya Ijumaa mjini Tehran na kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini. Iran imedai Israel na Marekani ndio waliotekeleza mauaji hayo. 

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwahi kumtaja Fakhrizadeh kama mkuu wa mpango wa awali wa siri wa silaha za nyuklia nchini Iran ulioitwa Amad. 

Iran ililazimika kusitisha mpango huo kutokana na shinikizo la kimataifa lakini bado haijatupilia mbali mipango yake ya nyuklia. 

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab amesema wanawasiwasi juu ya hali ilivyo nchini Iran na ukanda mzima wa Mashariki ya Kati baada ya kuwawa kwa Mohsen Fakhrizadeh.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *