img

Shambulizi la kundi la DAESH Iraq

November 29, 2020

 

Mtu mmojaameripotiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi lililoendeshwa na kundi la kigaidi la DAESH karibu na wilaya ya Şırgat katika mji wa Salahaddin nchini Iraq.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Salahaddin, iliarifiwa kuwa bomu lililokuwa limetegwa kwenye eneo la karibu na shamba wilayani Şırgat, lililipuliwa na wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi kwa kidhibiti cha mbali. Mkulima mmoja aliuawa katika kwenye mlipuko huo.

Miili ya watu 2 kutoka wilayani ilipatikana kwenye eneo la vijiji vya nje ya wilaya, masaa 3 baada ya watu hao kuchukuliwa mateka na wanamgambo wa DAESH.

Vikosi vingi vya usalama vilitumwa kudhibiti hali ya usalama katika eneo hilo baada ya tukio na operesheni ikaanzishwa dhidi ya wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi.

Mnamo mwezi Juni mwaka 2014, DAESH iliteka maeneo yote ya Mosul, Salahaddin na Enbar nchini Iraq , na pia baadhi ya sehemu za Diyala na Kirkuk, ambapo baada ya miaka kadhaa wakaikomboa kutoka mikononi mwa kundi hilo.  

Waziri Mkuu wa zamani Haydar al-Ibadi alitangaza ushindi dhidi ya DAESH mnamo Desemba 9, mwaka 2017.

Ingawa imepita takriban miaka 3 tangu Iraq ilipoondoa DEASH, kundi hilo bado limeonekana kuendeleza mashambulizi katika maeneo ya vijiji vya kanda hiyo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *