img

Raia wanne wapoteza maisha kwenye mlipuko wa vilipuzi Azerbaijan

November 29, 2020

Raia 4 wa Azerbaijan wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mlipuko wa vilipuzi vilivyowekwa na Armenia.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Azerbaijan, iliripotiwa kwamba gari moja lililpuliwa baada ya kupita kwenye eneo la vilipuzi vilivyotegwa katika kijiji cha Aşağı Seyitahmetli katika mkoa wa Fuzuli, ambao ulikombolewa kutoka mikononi mwa uvamizi wa Armenia mnamo 21 Oktoba.

Taarifa zaidi zimebainisha kuwa raia 4 waliokuwemo kwenye gari hilo walifariki kutokana na mlipuko.

Iliarifiwa kuwa mlipuko huo ulitokana na vilipuzi vilivyotegwa na wanajeshi wa Armenia walioondoka kwenye eneo hilo na vilikuwa ni vilipuzi vya kuzuia vifaru vya kijeshi

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *