img

‘Nyumba iliyochini ya ardhi ilikuwa makazi ya Yesu’, Wasema wanaakiolojia

November 29, 2020

Dakika 1 iliyopita

Rock-cut doorway entrance to the 1st Century house carved out of a natural cave

Maelezo ya picha,

Eneo la mlangoni lilikuwa limechongwa kwa kutumia jiwe lililokuwepo hapo

Wanaakiolojia “wanaamini” kuwa nyumba iliyojengwa chini ya ardhi huko Nazareth, Israel, ilikuwa makazi ya utotoni ya Yesu, kulingana na wachimbuzi wa vitu vya kale.

Profesa Ken Dark, kutoka chuo kikuu cha Reading, ametumia miaka 14 akisomea mabaki ya karne ya kwanza chini ya eneo la kidini la sasa.

Profesa huyo anasema kuwa mabaki yaliyofanyiwa utafiti, mwanzo yalionesha eneo hilo lilikuwa makazi kwa Yesu, Mary na Joseph karne ya 19.

Hata hivyo, hilo lilitupiliwa mbali na wanaakiolojia miaka 1930.

Eneo hilo likasahaulika kabisa tangu wakati huo hadi Profesa Dark alipoanza mradi wake wa kuhuisha tena mji huo mwaka 2006.

Alisema: “Sikwenda Nazareth kutafuta yaliyokuwa makazi ya Yesu, badala yake nilikuwa ninasomea historia ya hija ya Kikiristo ya Byzantium.

“Hakuna aliyepatwa na butwaa kama mimi.”

‘Utafiti ambao tunaweza kuufikia’

Alisema eneo hilo la kale lilikuwa chini ya kanisa enzi ya Byzantium.

Aidha, Profesa Dark anaelezea: “Tunachojua kutoka kwa ushahidi ulioandikwa, kanisa hili linaaminika kuwepo wakati wa Byzantium na lilijengwa katika eneo la makazi ya Yesu chini ya ardhi lililochimbwa na kuhifadhiwa mfano wa kaburi.

“Ni eneo lililokuwa Kanisa la Nutrition, lililotajwa katika hija ya karne ya 7.”

Profesa Dark anasema kazi yake imetambua nyumba hiyo kama iliyokuwepo karne ya kwanza na kugundua kuwa jengo hilo lilikuwa mfano wa pango kwenye vilima vyenye miamba.

Alisema yule aliyejenga nyumba hiyo, alikuwa na ufahamu mzuri wa kazi inayotumia jiwe ambaye wakati huo alijulikana kama tekton, jina la kale la fundi stadi lililotumika kumtambua Joseph katika bibilia.

Hata hivyo, wanaakiolojia hao walisema ingawa yote hayo huenda yasidhihirishe kwamba ilikuwa nyumba ya Yesu, “huo ndio utafiti unaoweza kufikia katika kusema hiyo ilikuwa nyumba ya Yesu”.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *