img

Maandamano dhidi ya Lukashenko yaanza tena mjini Minsk

November 29, 2020

Waandamanaji wa upinzani wamerejea tena barabarani katika mji mkuu wa Belarus Minsk katika maandamano ya hivi karibuni ndani ya miezi mitatu ya maandamano dhidi ya ushindi wa rais Alexander Lukashenko. 

Tangu kufanyika kwa uchaguzi wa Urais mwezi Agosti, Belarus imekumbwa na maandamano makubwa yaliotokea baada ya Lukashenko aliye na miaka 66 aliposhinda muhula wake wa sita madarakani katika taifa hilo la zamani la kisovieti. 

Upinzani unaamini uchaguzi ulikuwa wa udanganyifu na kiongozi wao Svetlana Tikhanovskaya –mpinzani wa Lukashenko aliegombea kwa kuchukua nafasi ya mumewe aliyekamatwa ndio mshindi halali wa uchaguzi huo. 

Katika miezi ya hivi karibuni serikali imekuwa ikiwakamata waandamanaji na kuzuia mkusanyiko wa aina yoyote mjini Minsk. Lakini kulingana na vyombo vya habari vya Belarus, maandamano takriban 20 yalirekodiwa hii leo mjini Minsk.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *