img

Kiongozi wa upinzani atiwa mbaroni Togo

November 29, 2020

Habari hiyo ni kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa umma. Taifa hilo lenye jumla ya watu milioni nane, linaongozwa na Rais  Faure Gnassingbe, ambae aliinfia madarakani 2005 kufuatia kifo cha baba yake Gnassingbe Eyadema, ambae alilitawala taifa hilo kwa miaka 38.

Kupitia televisheni ya umma Mwendesha Mashitaka,  Essolissam Poyodi alitangaza kukamatwa kwa mpinzani Brigitte Adjamagbo-Johnson kulikofanyika mjini Lome. Alisema hatua hiyo ilitokana na uchunguzi uliobaini nyaraka za upinzani zilizokuwa na mipango ya kuondoa hali ya utulivu wa nchi.

Wapinzani wanapinga matokeo ya urais wa Febururi, kwa kusema yaligubikwa na ulaghai

Togo Präsidentschaftswahl in Lome l Wahllokal

Mpiga kura akihakiki jina lake mjini Lome

Kwa upande wa ndugu wa mwanasiasa huyo waliliezea shirika la habari la Ufaransa AFP, kwambna ndugu yao alitiwa mbaroni akiwa nyumbani, kabla hajapelekwa katika Kituo cha Utafiti na Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.

Ijumaa iliyopita mpinzani mwingine, Gerad Djossou, vilevile alitiwa mbaroni. Poyodi aliongeza kusema baada ya kufanyika upekuzi nyumbani kwake Jumamosi waliweza kubaini kile walichosema kuwa ni mpango wa kufanya vitendo vya vurugu katika maandamano yaliopangwa kufanyika Jumamosi.

Soma zaidi:Faure Gnassingbe ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais

Upinzani uliitisha maandamano mjini Lome kwa lengo la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Februari, lakini yalisitishwa na serikali kwa sababu ya kuhatarisha maisha ya watu kutokana na janga la corona. Taifa hilo limerekodi maambukizi 1,722 na vifo vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *