img

CCM yawakaribishwa waliofukuzwa upinzani

November 29, 2020

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewakaribisha wanawake kutoka vyama vya upinzania kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa milango iko wazi kupokea wanawake wapambanaji na wenye nia ya kulitumikia taifa.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo Novemba 29, 2020 jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushahidi.

“Upinzani walikuwa na wakina Mama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni CCM milango iko wazi”, amesema Dkt. Bashiru.

Akizungumzia suala la ushindi wa Chama, “Hatuna mitambo ya kuiba Kura sisi kama Marekani, sisi mitambo yetu ni mabalozi wetu ambao walifanya kazi Usiku na mchana sababu tulikuwa tunashindana na vyama vilivyoishiwa sera. Vyama vimeshindwa kwa halali vinatafuta sababu kuna Watu wametukana siku 60 za kampeni badala ya kumwaga sera, niwapongeze sana Vijana wa Chama cha Mapinduzi mmeonesha uvumilivu sana kipindi chote cha kampeni”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *