img

Watoto wa mitaani waomba kukatiwa bima

November 28, 2020

Jukwaa la watoto na vijana kutoka mikoa sita nchini, wanaoishi na kufanya kazi mitaani, wameiomba serikali kuwasaidia kuwakatia bima ya afya ikiwemo kupatiwa ulinzi na usalama kutokana na kubaguliwa mtaani huku vyombo vya dola likiwemo Jeshi la polisi likiwachukulia kama wahalifu.

Kauli hiyo wameitoa katika mkutano wa jukwaa la watoto na vijana jijini Mwanza, uliojumuisha viongozi kutoka Wizara ya Afya, ulioandaliwa naa shirika la Railway children Africa kwa lengo la kutoa maoni na mapendekezo kwa serikali ili kuweza kupatiwa msaada na kuweza kuondokana na maisha magumu katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Railway Children Africa, Mussa Mgata, amesema kuwa mkakati wa shirika hilo ni kuhakikisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wanaondoka kabisa na kuwa na maisha bora.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi idara ya mtoto, ameomba mabaraza ya watoto yaliyopo nchini kuyafanyia kazi maoni ya watoto kuliko kuyapuuza, huku afisa maendeleo ya jamii Mwanza, akilishukuru shirika hilo kwa kuendelea kuwapa watoto elimu ya kuwaondoa mitaani na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *