img

Uingereza na Jumuiya ya Ulaya bado zatofautiana kifikra kwenye masuala mbalimbali

November 28, 2020

Jumuiya ya Ulaya (EU) imesema kuwa bado kuna hali ya kupishana kifikra kuhusu uhusiano wao wa baadaye na mazungumzo ya makubaliano ya biashara na Uingereza.

Mpatanishi Mkuu wa Brexit wa EU (Kuondoka kwa Uingereza kutoka EU) Michel Barnier, alitoa maelezo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii juu ya mazungumzo yanayoendelea kati ya EU na Uingereza.

Akiashiria ukosefu wa makubaliano kati ya pande zote kuhusiana na suala la uvuvi, msaada wa umma na suluhisho la mizozo ambayo inaweza kutokea baadaye, Barnier alisema,

“Tofauti muhimu za maoni na fikra zinaendelea. Tutakwenda London (mji mkuu wa Uingereza) jioni hii pamoja na timu yangu kuendelea na mazungumzo kati ya EU na Uingereza.”

Barnier alisema kuwa atawajulisha wawakilishi wa nchi za EU na Bunge la Ulaya (EP) leo hii juu ya hali ya mwisho ya mazungumzo.

Wiki iliyopita, mazungumzo ya Brexit yalisitishwa baada ya mmoja wa wawakilishi kukutwa na virusi vya corona (Covid-19), ambapo baadaye mazungumzo hayo yakaendeshwa tena kwa njia ya video.

Uingereza ambayo ilijiondoa rasmi EU tarehe 31 Januari, inafanya mazungumzo ya kina na muungano juu ya uhusiano wa pande zote mbili hasa katika suala la biashara.

Katika mazungumzo hayo kati ya EU na Uingereza, masuala ya “kuhakikisha ushindani”, “jinsi ya kusuluhisha mizozo ya kibiashara” na “uvuvi” ni yameleta tofauti zao za maoni na fikra.

Endapo makubaliano hayatawezi kufikiwa, uhusiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili utatekelezwa kwa kuzingatia sheria za Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) baada ya Desemba 31.

Katika kipindi chote cha mpito hadi tarehe hiyo, Uingereza inaendelea kuzingatia sheria za EU.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *