img

Mohsen Fakhrizadeh: Iran yaapa kulipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi wake

November 28, 2020

Dakika 5 zilizopita

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya video,

The road near Tehran where gunmen opened fire on Mohsen Fakhrizadeh

Rais wa Iran Hasan Rouhani amesema mauaji ya mwanasayansi wake wa masuala ya nyuklia hayatalemaza mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

Ameilaumu Israel kwa kuhusika na mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh nje ya mji mkuu wa Tehran, siku ya Ijumaa – akisema ilionesha wazi kiwango cha chuki na kubabaika kwa maadui wake.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo, lakini iliwahi kumshtumu mwanasayansi huyo kwa kuhusika na mpango wa kisiri wa kuunda silaha za nyuklia.

Makomanda wa kijeshi wa Iranwameapa kulipiza kisasi mauaji hayo.

“Kwa mara nyigine tena, mikono ya maadui wa ulimwengu waliojawa na kiburi wametuulia mtu wetu,” (maneno aliyotumia kuashiria Israel), Rais Hassan Rouhani alisema katika taarifa, kwa mujibu wa televisheni ya kitaifa.

“Mauaji ya shujaa Fakhrizadeh yanaonesha kuwa maadui wetu’ walivyotetereka na kiwango chao cha chuki dhidi yetu… Ushujaa wake hautarudisha nyuma mafanikio yetu.”

Fakhrizadeh alifariki hospitali baada ya kushambuliwa mjini Absard, katika kaunti ya Damavand.

Hossein Dehghan, mshauri wa kijeshi wa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameapa “kuwashambulia” walitekeleza mauaji hayo kama radi.

Iran inasisitiza mpango wake wa nyuklia ni salama na lengo lake ni la amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, amelaani mauaji hayo nakusema kuwa ni “kitendo cha ugaidi wa kitaifa -an act of state terror”.

Mashirika ya ujasusi ya magharibi yanaamini Fakhrizadeh alikuwa anasimasimamia mpango wa kisiri wa uundaji silaha za nyuklia za Iran.

“Endapo Iran ingeliamua kuunda silaha za nyuklia, Fakhrizadeh angelifahamika kama baba wa mabomu ya Iran,” mmoja wa wanadiplomasia wa Magharibi aliambia shirika la habari la Reuters mwaka 2014.

Lakini taarifa ya mauaji hayo zinajiri wakati kumekuwa na hofu mpya kuhusu uzalishaji wa madini ya urani unaofanywa na nchi hiyo.

Madini ya urani ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa kawi ya nyuklia na silaha za kijeshi za nyuklia.

Prominent Iranian scientist Mohsen Fakhrizadeh in an undated photo

Maelezo ya picha,

Mohsen Fakhrizadeh, alikuwa mkuu wa kitengo cha utafiti na uvumbuzi katika wizara ya ulinzi

Mkataba wa mwaka 2015 uliofikiwa na nchi sita zener uwezo duniani uliweka kiwango cha ukuzaji wa madini hayo, lakini tangu Rais Donald Trump alipojiondo katika mkataba huo mwaka 2018, Iran imekiuka makusudi makubaliano hayo.

Joe Biden amekubali kushauriana upya na Iran atakapoingia rasmi madarakani mwezi Januari kuwa rais wa Marekani, licha ya Israel kupinga hatua hiyo kwa muda mrefu. e longstanding opposition from Israel .

Kati ya mwaka 2010 na 2012, wanasayansi wanne wa nyuklia wa nchi hiyo wameuawa na Iran imelaumu Israel kwa kuhusika na mauaji hayo.

Jina la Fakhrizadeh lilitajwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika maelezo yake kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran mwezi April mwaka 2018.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa za mauaji ya mwanasayansi huyo.Pentagon pia imekataa kutoa kutoa kauli yoyote, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Ni nini kilimkuta Mohsen Fakhrizadeh?

Katika taarifa siku ya Ijumaa, wizara ya ulinzi ya Iran ilisema: “Magaidi waliyojihami walilenga gari lililokuwa limembeba Mohsen Fakhrizadeh, mkuu wa wizara hiyo katika shirika la utafiti na uvumbuzi.

“Baada ya makabiliano kati ya magaidi hao na walinzi wake, Bwana Fakhrizadeh alijeruhiwa vibaya ba kukimbizwa hospitali.

“Kwa bahati mbaya jitihada za madaktari kuokoa maisha yake hazikufabikiwa na muda mfupi baadaye akafariki.”

Map showing Absard and location of killing of Mohsen Fakhrizadeh

Taarifa za vyombo vya habari nchi Iran zinasema washambuliaji walimiminia risasi gari la mwanasayansi huyo.

Shirika la habari la Fars awali liliripoti kuhusu mlipuko wa gari katika mji wa Absard, huku waliyoshuhudia tukio hilo wakdai kuwa “watu watatu hadi wanne waliyodaiwa kuwa magaidi wakiuawa”.

2px presentational grey line

Kwanini alilengwa?

Kama mkuu wa wizara ya ulinzi katika kitengo cha utafiti na uvunmbuzi, Fakhrizadeh bila shaka alikuwa kiungo muhimu. Ndio maana Benjamin Netanyahu alitoa onyo, miaka miwili iliyopita “wakumbuka jina lake”.

Tangu Iran ilipoanza kukiuka utekelezaji wa mktaba wa nyuklia uliyofikiwa mwaka 2015, nchi hiyo imeendelea mbele na hatua ya kukuza madini ya urani kuimarisha uzalishaji huo kupita kiwango kilichokubailiwa.

Maafisa wa Iran wamekuwa wakisema hatua kama hizo zinaweza kurudishwa nyuma lakini utafiti na maendeleo ni vigumu kufutilia mbali.

“Hatuwezi kurudi nyuma,” Balozi wa zamani wa Iran katika Shirika la Kimataifa la Kawi ya Atomiki (IAEA), Ali Asghar Soltanieh, alisema hivi karibuni.

Ikiwa Mohsen Fakhrizadeh alikuwa kiungo muhimu kama vile Israel inavyodai, basi mauaji yake yanaashiria jaribio la kupunguza kasi ya Iran kuendelea mbele na mpango wake wa nyuklia.

Huku rais mteule wa Marekani, Joe Biden, akizungumzia mpangio wa kurudisha Washington katika mkataba wa nyuklia wa Iran, mauaji ya mwanasayansi huyo huenda yalilenga kusambaratisha majadiliano yoyote ya siku zijazo kuhusu suala hilo.

2px presentational grey line

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *