img

Marekani yawekea vikwazo Urusi na China

November 28, 2020

 

Marekani imechukuwa uamuzi wa kuweka vikwazo dhidi ya mashirika ya Urusi na China. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kuwekea vikwazo mashirika ya Urusi na China, kufuatia Kanuni ya Uvujishaji wa Silaha kwa nchi za Iran, Korea Kaskazini na Syria. 

Nchi zote mbili zinatuhumiwa kwa madai ya kuruhusu mashirika yao kutuma vifaa na vyombo vyenye miundo nyeti ya teknolojia ya makombora kwa nchi ya Iran. 

Hatua hiyo imechukuliwa ili kuzitaka nchi hizo kuepukana na utoaji wa vifaa na bidhaa za aina yoyote zinazoweza kusaidia utengezaji wa makombora nchini Iran. 

Maelezo yaliyotolewa pia yalisisitiza kwamba vikwazo vitaendelea kuwekwa dhidi ya wauzaji wa kimataifa kwa lengo la kuzuia utengezaji wa makombora Iran. 

Vikwazo hivyo vimetangazwa kuwa vitadumu kwa kipindi cha miaka 2. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *