img

Mapacha waliounganika: ‘Tulijua kuwa tuko tofauti na watoto wengine’

November 28, 2020

Dakika 7 zilizopita

Sanchia and Eman Mowatt

Maelezo ya picha,

Mapacha Sanchia na Eman Mowatt

Mwezi Decemba mwaka 2001, upasuaji hatari wa kuwatenganisha mapacha wa miezi mitatu waliozaliwa wakiwa wameunganika ulifanyika katika hospitali moja mjini Birmingham, Uingereza.

Sanchia na Eman Mowatt walianza safari yao ya maisha baada ya upasuaji huo ambao uliangaziwa na vyombo vya habari kote duniani.

Je maisha kwa mapacha hao ambao sasa wana umri wa miaka 19 yanaendeleaje?

Mmoja wa madaktari katika chumba cha upasuaji “alisema neno la kitaalamu” ambalo lilifanya kundi zima la madaktari waliokuwa katika chumba hicho kushangilia kwa vigelegele.

Hatimaye baada ya upasuaji huo ambao ilichukua takriban saa 16, watoto hao wachanga wa kike walitenganishwa salama.

Walikuwa wameishi miezi mitatu wakiwa wameunganika katika sehemu ya uti wa mgongo.

Upasuaji huo ulikuwa hatua kubwa ya tiba katika hopotali ya watoto ya Birmingham – ulikuwa wa kwanza kufanyika chini Uingereza na kufanyika mara ya tatu duniani.

Pia ulikuwa upasuaji hatari zaidi – uwezekano wa mapacha hao kufa baada ua kutenganishwa ulikuwa kati ya asailimia 5 na 25%.

Hata baada ya upasuaji kulikuwa na hofu mmoja kati ya mapacha hao angefariki au wote wawili huenda wangelipooza baada ya kwasababu ya kuwatenganisha sehemu ya uti wa mgongo.

Lakini kwa bahati nzuri upasuaji huo ulikamilika salama. Sanchia na Eman waliponea kifo na wazazi wao Emma na David hatimaye wanaweza kuwabeba wakiwa wametenganishwa.

Vyombo vya habari viliwaangazia wazazi hao kwa mara ya kwanza wakiwa wamebeba watoto wao kila mmoja.

Emma and David Mowatt holding their daughters.

Maelezo ya picha,

Sanchia na Eman sasa ni wanafunzi wa chuo kikuu. Dada yao Damaris ambaye alizaliwa miezi 11 baadae amekuwa pamoja nao katika safari ya maisha ya kawaida ya mapacha hao.

“Watu hawaangazii sana kuhusu kisa cha kuzaliwa kwetu tukiwa tumeshikamana, lakini ni kitu tumezoea,” anasema Eman, akikumbuka maisha yao walipofika duniani.

Madaktari walikuwa wametabiri kwamba mapacha hao wataishi maisha ya kawaida wakitenganishwa salama.

Wote wanatumia kifaa kilichowekwa katika sehemu ya uti ea mgongo ili kuwasaida kwa matembezi huku kila mmoja waovakiwa na mguu ambao uko hafifu. Haikujulikana kama hali hiyo ingeleathiri ukuaji wao.

“Hawakujua kama tungeliweza kutembea baada ya kufanyiwa upasuaji huo,” anasema Sanchia. “Tulianza kutembea, watu walisema ni miujiza.”

The twins in hospital

Ni Sanchia ambaye alianza kutembea akiwa na miaka miwili, naye Eman akafuatia wiki tano baadaye. Kabla ya muda mrefu, watoto hao walikuwa wakikimbia na kucheza katika boma la wazazi wao mjini Birmingham.

Maisha yao ya utotoni ilikuwa mchanganyiko wa kusoma shule ya msingi na safari za kwenda hospitali na kushiriki vipindi vya televisheni kujadili wanavyoendelea baada ya kufanyiwa upasuaji.

“Tulijua tuko tofauti na watoto wengine tukiwa na umri mdogo – pia tulijua kuhusu tarehe ya kwenda hospitali, upasuaji, na kwamba hatukuwa na uwezo wa kufanya kila kito ambacho watoto wenzetu wanafanya,” Eman kumbukumbu yake, japo anasema wanafunzi wenzao wadogo darasani “walielewa sana” hali yao na walifurahia kuwa marafiki zao na kusalia hivyo hadi wa leo.

Twins and Damaris in the garden

Wanasema mguu wao uliyodhaifu unamaanisha mahali ambapo ni mwendo wa dakika tano huenda ukawachukua dakika 20 -na wanalazimika kutumia kiti cha magutudumu ama crutch.

“Tulikubali hali yetu ya ulemavu tukiwa na umri mdogo,” anasema Sanchia. “Hatukumruhusu mtu yeyote atuambie hatuwezi kufanya kitu.”

Anatoa mfano kutoka siku zao wakiwa wadogo shuleni.

“Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka minne nikijihisi kuwa tofauti,” anasema. “Tulikuwa tunacheza na playing tig alafu mtoto mmoja maulana akaniambia ‘huwezi kucheza mchezo wa kukimbia kwasababu ya mguu wako’.

“[Nikajiambia] ‘ndio, nina ulemavu lakini mtu hastahili kukwambia kile unachoweza kufanya ni kile ambacho huwezi kufanya’. Siku hiyo nilikimbia, sikufanya vyema lakini nilikimbia.

“Mtu akikwambia kitu kama hicho anakupatia motisha na msukumo wa kusema ‘ndio naweza!””

Line

Upasuaji uliotakiwa kufanyiwa Sanchia na Eman ulikuwa wa kutenganisha uti wao wa mgongo uliokuwa umeshikamana sehemu ya chini, upasuaji ambao haukuwa umewahi kufanyika nchini Uingereza.

Wataalamu wa upasuaji wakiongozwa na Tony Hockley walitenganisha uti wa mgongo na viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na vibofu vya mkojo.

Akielezea upasuaji huo baadaye, Bwana Hockley aliambia gazeti la The Guardian: “Wawili hao walikuja pamoja wakashikana wakati wa kugeuka. Ilibidi tukate sehemu hiyo ili kila mtoto asalie na uti wake wa mgongo, na kuwatengezea mpira maalum ya kufunika sehemu hiyo.

The scan of the girls before they separated

Baada ya uti wa mgongo kutenganishwa, daktari wa upasuaji wa watoto na mmoja wa wataalamu wa kutenganisha mapacha walioshikamana duniani , Peter Gornall na Lewis Spitz nchini Uingereza walifanya oparesheni ya kutenganisha viungo vya watoto hao ambavyo vilikuwa kamili lakini vimeshikana pamoja.

Katika maisha ya ujana wao mapacha hao, wamekuwa kijaribu kuweka siri historia yao, lakini wanafunzi wenzao hushangaa sana wanapowaelezea kuhusu maisha yao.

“Watu waliyaka sana kujua – wangeliutuuliza, kama ni kweliis? Lakini tulitaka suala hilo liwe la faragha,” anasema Sanchia. “Walifuatilia halibyetu mtandaoni. Nilidhani watu wataacha kuzungumza- nikidhani ni wingu la kupita- lakini hawakuacha kufanya hivyo.”

Wanamuenzi sana daktari aliyewafanyia upasuaji huo, Tony Hockley,ambaye amekuwa mwandani wa karibu wa familia yao.

Anakumbuka kila mwaka wao wa kuzaliwa na amekuwa akiwatembelea mara kwa mara nyumbani kwao.

Daktari huyo alifariki ghafla mwaka 2009, akiwa na umri wa miaka 65, na mwaka jana mapacha hao walihudhuria hafla ya ukumbusho wake, hatua ambayo ilifariji sana familia yake na wafanyakazi wenzake.

Line

Uhusiano kati ya Hospitali ya watoto ya Birmingham na mapacha hao Sanchia na Eman umeimarika zaidi wipokuwa wakubwa.

Kiasi cha kuwa wote wawili walifanya mazoezi ya kazi wakiwa wanafunzi hapo, na kukutana na baadhi ya wahudumu wa afya katika chumba cha upasuaji waliyo wahudumia miaka 16 iliyopita.

The twins in scrubs

Ilikuwa raha sana” anasema Sanchia. “Tulimuona daktari aliyetudunga sindano ya ganzi wakati huo, yule aliyetusaidia na kifaa cha kupumulia na wanafunzi waliokuwa wanasomea udaktari wakati tulipozaliwa.

“Ulikuwa wakati mzuri sana na wa kutia moyo. Tunachukulia nafasi hii kwa umuhimu mkubwa.”

Masomo yao yalikatizwa kutokana ba jsnga la corona, ambaho ililazimisha shule yao kufungwa mwezi Machi.

Licha ya janga ka corona mapacha hao na dada ya Damaris ambaye wanasoma paomoja shule moja wana matumaini wataendelea na masomo yao.

Waliandaa dhifa ya kujumuika na marafiki kupitia mfumo wa mawasiliano ya kidijitali wa Zoom.

“Ilikuwa siku nzuri sana,” anasema Eman. “Hivyo ndivyo tuliamua kufunga mwaka wetu wa shule kwa kucheza ndani densi ndani ya sebule yetu.”

Twins

Line

Mapacha waliounganika

Sanchia and Eman shortly after they were born

•Huwa wanafsnana kwasababu wametokana na yao moja

•Ni nada jana kupa mapacha walioungana, wanakadiriwa kuwa moja kati ya karibu mapacha 200,000 wanaozaliwa.

•Mara nyingi huunganika sehemu ya kifua, tumbo au nyonga

•Karibu asilimia 70% y amapacha waliounganika ni wa kike

•Kumekuwa na nadharia miili kwanini wanaunganika:

Huenda mgawanyiko katika viinitete viwili hulifanyika baadaye kuliko kawaida, na mapacha wakagawanyika kidogo, au sehemu za viinitete vilivyobaji viliendelea kuwasiliana na sehemu hizo za mwili huungana kadri zinavyokua.

Line

Wote watatu sasa wako chuo kikuu. Sanchia anasomea usalama mtandaoni, Eman siasa na uhusiano wa kimataifa, na Damaris is doing childhood, youth and educational studies.

Sanchia pia anajifunza jinsi ya ku code kama sehemu ya azma yake ya kuwavutia wanawake weusi kujiunga na masuala ya teknolojia.

“Watu weusi wanahitaji zaidi kujifunza mambo ya teknolojia,” anasema. “Mimi ni msichana wa Caribbean – huwaoni bsadhi yao [katika kazi hii]. Nataka kuleta mabadiliko na kujiridhisha mwenywe kwamba inawezekana na ninaweza kufanya.”

Naye Eman, ana ndoto ya kuwa mwanasiasa, akitoa mfano wa mwanasiasa wa Marekani Alexandria Ocasio-Cortez kuwa mtu anayemvutia. “Kizazi kipya cha wanasiasa kitakuwa tofauti – tunaishi katika ulimwengu unaoendelea kubadilika,” anasema.

Mapacha hao wanafahamu fika kwamba maisha yao yanatokana na kuponea upasuaji hatari waliyofanyiwa wiki za mwanzo wa maisha yao duniani, lakini wanajichukulia kama wanawake wa kawaida- walio na ndoto kubwa na dunia inayozunguka familia yao, marafiki na imani yao.

“Lazima umshukuru Mungu kwa uhai katika maisha yako….,” anasema Eman.

“Tumesoma kuhusu mapacha wengine [ambao walifariki],” aliongezea Sanchia. “Inasikitisha sana. Sisi pia huenda tungelifariki.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *