img

Mahakama ya Pennsylvania yakataa ombi la Trump

November 28, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump amepokea majibu yasiyoridhisha kutoka mahamaka ya Pennsylvania kufuatia malalamiko ya kisheria aliyowasilisha juu ya matokeo ya uchaguzi wa urais wa 59 uliofanyika Novemba 3 nchini humo. 

Juhudi za timu ya Trump ambayo hapo awali ilikataliwa ombi lao wailowasilisha kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais katika jimbo hilo na kuamua kupeleka kesi mahakama ya rufaa ya Pennsylvania, pia ziliambulia patupu. 

Mahakama ya rufaa ya Philadelphia ambao ni mji mkuu wa Pennsylvania, ilitangaza kukataa malalamiko yanayodai kuwa uchaguzi uliokuwa na udanganyifu kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha. 

Timu ya Trump ilitoa maelezo kuhusu uamuzi huo na kusema kuwa watawasilisha kesi yao katika mahakama ya juu ya Marekani. 

Wiki iliyopita, kesi hiyo iliwasilishwa na kusikizwa katika mahakama ya chini ambapo wakili wa Trump Rudy Giuliani, alidai kuwa uchaguzi ulihusishwa na visa vya udanganyifu na wataendeleza mapambano yao hadi mwisho wa kesi hii.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyopo, mgombea wa chama cha Democrats Joe Biden, ana haki ya kuingia madarakani kwa kupata wajumbe 306 dhidi ya Trump aliyepata wajumbe 232 na kupinga matokeo ya uchaguzi. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *