img

Kiongozi wa Hong Kong afungiwa akaunti ya benki

November 28, 2020

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amefungiwa akaunti yake ya benki baada ya Marekani kumuwekea vikwazo vya kiuchumi, ikimuadhibu kwa kutangaza sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyoamrishwa na China bara. 

Lam amewekewa vikwazo hivyo pamoja na wenzake 14, wote wakiwa maafisa wa ngazi za juu mjini Hong Kong. Vinatajwa kuwa ni vikwazo vikali kuwahi kuwekewa Hong Kong tangu ilipotangaza sheria hiyo mpya ya China mnamo mwezi Juni. 

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Hong Kong HKIBC jana usiku, Lam amesema amelazimika kutumia fedha taslim kwa ajili ya mahitaji yake yote. 

Lam ni mmoja wa viongozi wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi ulimwenguni wa dola 672,000. Aliviambia vyombo vya habari mnamo mwezi Agosti kwamba anakabiliwa na usumbufu kutokana na vikwazo hivyo ambavyo vimemkwamisha kutumia kadi zake za benki.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *