img

Iran yasema italipiza kisasi kifo cha mwanasayansi Fakhrizadeh

November 28, 2020

Rouhani aliilaumu Israel kwa mauaji hayo akisema ni dhihirisho la wazi la kiwango cha chuki na kubabaika kwa maadui wa Iran.

“Kwa mara nyigine tena, mikono ya maadui wa ulimwengu waliojawa na kiburi umetuulia mtu wetu,” Rouhani alisema katika taarifa, kwa mujibu wa televisheni ya kitaifa.

Rais huyo hata hivyo alisema kuuawa kwa mwanasayansi huyo, hakutalemaza juhudi za Iran za kwendelea na mpango wake wa kuimarisha uzalishaji wa nyuklia, suala ambalo, kwa miaka kadhaa sasa, limeibua changamoto za diplomasia ya kimataifa.

Licha ya kushutumiwa kwa kuhusika kwa kifo cha Fakh-rizade, Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo, lakini iliwahi kumshtumu mwanasayansi huyo kwa kuhusika na mpango wa kisiri wa kuunda silaha za nyuklia.

Fakhrizadeh alifariki hospitali baada ya kushambuliwa mjini Absard, katika kaunti ya Damavand.

Wakati huo huo, Hossein Dehghan, mshauri wa kijeshi wa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameapa “kuwashambulia walitekeleza mauaji hayo kama radi.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *