img

Iran yaapa kulipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi wake

November 28, 2020

Rais wa Iran Hasan Rouhani amesema mauaji ya mwanasayansi wake wa masuala ya nyuklia hayatalemaza mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

Ameilaumu Israel kwa kuhusika na mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh nje ya mji mkuu wa Tehran, siku ya Ijumaa – akisema ilionesha wazi kiwango cha chuki na kubabaika kwa maadui wake.

Israel haijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo, lakini iliwahi kumshtumu mwanasayansi huyo kwa kuhusika na mpango wa kisiri wa kuunda silaha za nyuklia.

“Kwa mara nyigine tena, mikono ya maadui wa ulimwengu waliojawa na kiburi wametuulia mtu wetu,” (maneno aliyotumia kuashiria Israel), Rais Hassan Rouhani alisema katika taarifa, kwa mujibu wa televisheni ya kitaifa.

“Mauaji ya shujaa Fakhrizadeh yanaonesha kuwa maadui wetu’ walivyotetereka na kiwango chao cha chuki dhidi yetu… Ushujaa wake hautarudisha nyuma mafanikio yetu.”

Fakhrizadeh alifariki hospitali baada ya kushambuliwa mjini Absard, katika kaunti ya Damavand.

Hossein Dehghan, mshauri wa kijeshi wa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameapa “kuwashambulia” walitekeleza mauaji hayo kama radi.

Iran inasisitiza mpango wake wa nyuklia ni salama na lengo lake ni la amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, amelaani mauaji hayo nakusema kuwa ni “kitendo cha ugaidi wa kitaifa -an act of state terror”.

Mashirika ya ujasusi ya magharibi yanaamini Fakhrizadeh alikuwa anasimasimamia mpango wa kisiri wa uundaji silaha za nyuklia za Iran.

“Endapo Iran ingeliamua kuunda silaha za nyuklia, Fakhrizadeh angelifahamika kama baba wa mabomu ya Iran,” mmoja wa wanadiplomasia wa Magharibi aliambia shirika la habari la Reuters mwaka 2014.

Lakini taarifa ya mauaji hayo zinajiri wakati kumekuwa na hofu mpya kuhusu uzalishaji wa madini ya urani unaofanywa na nchi hiyo.

Madini ya urani ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa kawi ya nyuklia na silaha za kijeshi za nyuklia.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *