img

Idadi ya vifo vya corona Ulaya yapindukia 400,000

November 28, 2020

Zaidi ya watu 400,000 wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona barani Ulaya kulingana na takwimu za leo zilizokusanywa na shirika la habari la AFP, kutoka katika vyanzo rasmi vya kuaminika. 

Bara la Ulaya ni la pili liloathiriwa vibaya na maambukizi ya virusi hivyo baada ya Amerika Kusini na Karibiki. 

Watu wapatao 400,649 wamefariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19. Idadi hiyo ni kutoka miongoni mwa watu 17,606,370 waliothibitishwa kupata ugonjwa huo barani humo. 

Vifo 36,147 vimetokea katika wiki chache zilizopita. Inatajwa kuwa ni idadi kubwa zaidi ya vito kutokea barani Ulaya tangu janga hilo la maambukizi kuanza mwanzoni mwa mwaka. 

Nchi zinazoongoza kwa kuwa na maambukizi mengi ni Uingereza, ikifuatiwa na Italia, Ufaransa, Uhispania pamoja na Urusi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *