img

Wissmannstraße: Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania

November 27, 2020

Dakika 13 zilizopita

Barabara hiyo ya Wissmannstraße inatarajiwa kubadilishw ajina mwaka ujao

Maelezo ya picha,

Barabara hiyo ya Wissmannstraße inatarajiwa kubadilishw ajina mwaka ujao

Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja linalompatia heshima gavana mmoja wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika mashariki aliyeshutumiwa kwa kuagiza mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara ya Wissmannstraße, iliopatiwa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße.

Alikuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa hilo.

Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwasasa ndio mataifa ya Tanzania , Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakaazi wengi limetangaza gazeti la Ujerumani, Der Tagesspiegel .

Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko liliunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa.

Katika taarifa lilisema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa ”Von Wissmann na mahala pake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi”.

“Wissmann alikuwa mbaguzi na muhalifu wa kivita . Lucy Lameck anawakilisha mchango ulioshushwa thamani wa wanawake wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo”, alinukuliwa akisema mwanaharakati wa Tanzania Mnyaka Sururu Mboro.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *