img

Waziri wa Ujerumani ataka Wasyria warudishwe nyumbani

November 27, 2020

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Horst Seehofer amesema zuio la kuwarudisha wahamiaji wa Syria nyumbani halipaswi kuongezwa muda zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu. 

Katika mkutano ujao ambapo atakutana na viongozi wenzake kutoka majimbo yote 16 ya Ujerumani, Seehofer anatarajiwa kupendekeza kwamba kila mhamiaji kutoka Syria lazima kesi yake ichunguzwe tena ili kubainisha uwezekano wa kumrudisha nyumbani. 

Seehofer amesisita hilo lizingatiwe hasa kwa wahalifu, na wale wanaohofiwa kuwa tishio kwa taifa. Marufuku ya kuwarejesha nyumbani wahamiaji wa Syria ilipitishwa Ujerumani mnamo mwaka 2012. Na tangu wakati huo imekuwa ikiongezewa muda. 

Na leo hii, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikipiganwa nchini Syria, vimemalizika katika sehemu nyingi nchini humo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *