img

Waziri Mkuu wa Ethiopia awaahidi wajumbe wa Afrika kuwalinda raia wa Tigray

November 27, 2020

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewaambia wajumbe wa Umoja wa Afrika kuwa serikali yake itawalinda raia wa jimbo la kaskazini la Tigray, siku moja baada ya kutangaza kuwa serikali inaanza awamu ya mwisho ya mashambulizi katika eneo hilo.

 Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wao haikutaja mazungumzo na Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray – TPLF ili kumaliza mapigano ambayo yalianza Novemba 4. 

Abiy amekutana leo na wajumbe wa Umoja wa Afrika – marais wa zamani Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, Joaquim Chissano wa Msumbizi na Kgalema Motlanthe wa Afrika Kusini na kuwaahidi kuwa serikali imedhamiria kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia. 

Serikali iliwapa wanajeshi wa TPLF hadi Jumatano kuweka chini silaha au wakabiliwe na mashambulizi katika mji mkuu wa jimbo hilo Mekelle, ambao una wakaazi nusu milioni hali iliyozusha hofu miongoni mwa mashirika ya misaada ya kutokea vifo vingi vya watu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *