img

Watu 53 wafariki kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen

November 27, 2020

Katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka 2020, kesi 204,291 za maambukizi za ugonjwa wa kipindupindu zilionekana nchini Yemen ambapo watu 53 walipoteza maisha.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya Twitter na ofisi ya Yemen ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), iliarifiwa kuwa watu 204,291 wanaoshukiwa kuwa kesi za maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu waligundulika nchini Yemen katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka.

Taarifa zaidi zilifahamisha kwamba watu 53 walifariki kutokana na visa vya ugonjwa wa kipindupindu, na kuelezwa kuwa WHO iliendeleza msaada wake wa serikali ya Yemen kwa ajili ya mapambano dhidi ya kipindupindu.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *