img

Washiriki 20 wa Shindano la Miss Tanzania 2020, waingia kambini

November 27, 2020

 Takribani washiriki (warembo) 20 wa Shindano la Miss Tanzania 2020, waingia rasmi kambini  katika hoteli ya Serene Mbezi Beach.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ambayo imepewa dhamana ya kuandaa Mashindano hayo (The look company)  amesema warembo hao wapatao 20 tayari wameingia kambini.

“Mchakato wa kupata washiriki ulifunguliwa rasmi Machi 2020 na tulianza usahili kwa Kanda ya Kati.” Mwanukuzi ameeleza jinsi gonjwa la covid 19 (Corona) lilivyoharibu mikakati yao wakati wanaenda kufanya usahili Kanda ya kaskazini.

“Kutokana na shida hiyo tulilazimika kuhamishia usahili kupitia online na kupata takribani washiriki 100 wenye vigezo, tuliwachuja warembo 50 na hatimae tukatapa warembo 20 ambao wameingia kambini rasmi.”

Aidha, ametaja Kanda ambazo zilijumuishwa katika mchakato wa kupatikana washiriki hao ni pamoja na Kanda ya ziwa, Kanda ya juu kusini, Kanda ya kati pamoja na Dar es salaam.

Pia amefafanua kuwa kwa mwaka huu kitu cha tofauti kwa warembo hao ni wameshaanza kuandaa mpango mkakati (project ) mapema kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka.

Muandaaji huyo ametaja zawadi kwa mshindi atakaepatikana siku ya fainali, ambayo ni gari aina ya Subaru pamoja na washiriki wengine watapata fedha, viatu pamoja na kitanda kutoka kwa wadhamini.

Sanjari na hilo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu spika wa bunge #TuliaAckson na Mashindano hayo yatafanyika desemba 5 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam. Bei ya tiketi ni kama ifuatavyo; 100,000, 65000, 50000 na 25000

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *