img

Wanaosema mume wangu mdogo wana kadi lake la kliniki?- Asha Boko

November 27, 2020

Msanii wa vichekesho kotoka hapa nchi Asha Boko amefunguka ukweli kuhusu ndoa ake na kuweka ukweli kuwa waliodhani ni movie au kiki ni uongo bali ni kweli wamefunga ndoa.

Asha Boko amedai kuwa alishawahi kuolewa na hii ni ndoa ya pili ila ile a kwanza akuachika bali mumewe aliuawa na majambazi.

“Hii ndoa yangu ya pili, Mume wangu wa kwanza hatukuachana na tulibahatika kupata watoto wawili na wakati tunakaa Kimara tulivamiwa na majambazi na alipigwa risasi na kupoteza maisha yake, ni miaka 13 imepita” Ashaboko

“Mume wangu mdogo wao wana kadi lake la clinic na sidhani kama wanatakiwa kujua umri wa mume wangu ila sababu labda yeye ni mwembamba na mwili wake mdogo anaonekana mdogo ila sio mdogo. Mwangalieni sura yake mkubwa anaonekana” Ashaboko

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *