img

Wajumbe wa Afrika kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia kuhusu Tigray

November 27, 2020

Wajumbe wa amani wa Umoja wa Afrika wanatarajiwa kukutana leo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, siku moja baada ya Abiy kusema kuwa jeshi linaanza awamu ya mwisho ya mashambulizi katika jimbo la kaskazini la Tigray ambayo mashirika ya haki yanahofia huenda ikasababisha hasara kubwa kwa raia.

 Msemaji wa Kikosi Kazi cha serikali cha Hali ya Dharura kuhusu mzozo wa Tigray Redwan Hussein amesema wajumbe hao walitarajiwa kukutana na Abiy mchana huu. 

Wakati huo huo, watu wanaendelea kuukimbia mji mkuu wa Tigray, Mekele wakihofia mashambulizi kamili ya vikosi vya shirikisho. 

Mapigano yameripotiwa kufanyika nje ya Mekele, mji wenye watu karibu nusu milioni ambao wameonywa na serikali ya Ethiopia kuwa hawatahurumiwa kama hawatojitenga na viongozi wa Tigray kwa wakati mwafaka kabla ya kuanza operesheni ya mwisho.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *